TEF: Hatuendi kuvutana na serikali



DEODATUS Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema wadau wa habari hawaendi kushikana mashati na serikali kwenye kikao chao cha tarehe 11 na 12 Agosti 2022.

Amesema, kikao hicho kitatumika kwa maslahi mapana ya wanahabari na vyombo vyao kwa kuwa, ndio safari ya kuelekea mabadiliko ya sheria za habari nchini.

Balile ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mtangazaji Abdallah Kurwa katika Kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One tarehe 10 Agosti 2022.


“Tunakwenda kwenye kikao cha serikali na wadau wa Habari si kwa lengo la kuvutana mashati, bali tunalenga kutengeneza mazingira bora ya tasnia ya habari. Kwa pamoja tunakwenda kuangalia maslahi ya mwandishi na wamiliki wa vymbo vya habari, lakini maboresho haya yanalenga zaidi uhuru wa kupata habari,” amesema. 

Pia amesema, kikao hicho kitapitia mapendekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya elimu katika tasnia ya habari.Katika hilo amesema, wanapendekeza waandishi waliopo kwenye tasnia ya habari ambao hawajafikisha vigezo, wasiondolewe na badala yake wapate mafunzo wakiwa kazini, huku wanaoingia lazima wakidhi vigezo vya elimu iliyoweka.


“Tungependa waandishi waliopo kazini wasiondolewe bali wapate mafunzo wakiwa kazini, lakini wale wapya wanaotaka kuingia katika tasnia ya habari, lazima wakizi vigezo vya kuwa na elimu walau Diploma,” amesema Balile,

Mwenyekiti wa TEF.Amesema, sio kila anayeweza kusoma na kuandika anaweza kuwa, na kwamba uandishi ni taaluma iliyo na misingi yake.
“Kuna kipaji na taaluma, ukiwa na kipaje basi lazima upate misingi ya taaluma hapo unakuwa mwandishi mzuri, kila taaluma ina misingi yake,” amesema.
Previous Post Next Post