WANAWAKE WA NJOMBE WAMPONGEZA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA UMOJA WA WANAWAKE(UWT).



WANAWAKE wa Mkoa wa Njombe wamempongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT) wa Mkoa huo Scholastika Kevela kwa kuiongoza vyema jumuiya hiyo na kuhamasisha maendeleo kwa wanawake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mkoani humo, wanawake hao hususani kutoka Chama cha mapinduzi walisema katika kipindi chote ambacho Jumuiya hiyo imekuwa chini ya mwenyekiti huyo  kwa kiasi kikubwa wameweza kuwa kitu kimoja na  kukiunganisha chama.

Mkazi wa Igandalamunyo kilichopo Wanging’ombe Eva Mbwilo amesema wanawake wa CCM wa Mkoa huo wamekuwa na umoja na utulivu katika kipindi amabacho Mwenyekiti huyo amekuwa akiwa mwenyekiti wao huku akisisitiza kuwa Jumuiya hiyo chini ya mwenyekiti huyo ipo imara sambamba na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kichama na kijamii.

“Amekuwa kiunganishi kizuri kati ya UWT dhidi ya Jumuiya zingine ndani na nje ya mkoa wetu jambo linalozidi kukihimarisha chama chetu, kimsingi kazi zake anazozifanya ndani ya Jumuiya zimekuwa zikionekana kwa macho kiasi cha kusema kuwa anamsaidia Rais Samia kutekeleza majukumu yake” amesema Mbwilo.

Aidha amesema wao kama wanawake wa mkoa huo wataendelea kumuunga mkono kwa kumpa ushirikiano wakati wote atakapokuwa anatekekeleza majukumu ya chama hicho ili kuendelea kukifanya chama hicho kuwa imara wakati wote na kuendeleza ushindi wake dhidi ya vyama vingine vya siasa.

Naye Sauda Sanga kutoka Kijiji cha Ikwega amemtaja Mwenyekiti huyo kuwa kiongozi shupavu na mwenye maono ya kuipeleka mbali Jumuiya huku huku akibainisha mambo mbalimbali aliyoyafanya ikiwemo kuwahamisha wanawake wa mkoa huo kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Amehamasisha mambo mbalimbali ndani ya mkoa wetu ikiwemo ya uanzishwaji wa kiwanda cha sabuni, kilimo cha parachichi na miradi mingine ambayo kimsingi yanatupa chachu ya maendeleo..haya ni maono ya  viongozi wachache katika Taifa hili, ukweli amekuwa akiendana na falsafa za Rais Samia Suluhu Hassan za kututaka tuchape kazi kupitia kauli  yake ya Kazi Iendelee” alisema Sanga

Amesisitiza wao kama wanawake wa mkoa huo wamejenga imani naye kwa kiasi kikubwa ya utendaji wake wa kazi na zaidi ameahidi kuwa naye bega kwa bega hasa pale anapotekeleza majukumu yake ya kichama ndani na nje ya mkoa Njombe

 
Previous Post Next Post