Rais Samia asisitiza viwanja vya kisasa kujengwa Dar



Na John Mapepele

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakwenda kujenga viwanja vya michezo ya ndani na maonesho ya Sanaa katika eneo la Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam ili wanamichezo wapate mahali bora kwa kufanyia mashindano na kuwavutia watu kufanyia mashindano makubwa ya kimataifa.



Kauli hiyo ameitoa leo Julai 05, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake chini ya Umri wa Miaka 17 ( Serengeti Girls) 
 na kuipongeza kwa kufuzu kucheza Kombe hilo.

Aidha, Mhe.Rais amesema dhamira ya Serikali ni kujenga miundombinu bora itakayosaidia kuboresha viwango vya wachezaji wetu.



Tukio hilo limepambwa na Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya akiwemo Barnaba na Frida Amani ambao waliotumbuiza kwa jumbe nzuri zilizomfanya Mhe. Rais kuwatunza.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu, Menejimenti ya Wizara na wadau mbalimbali wa michezo.
Previous Post Next Post