PETER MADUKI: VETA IMEJIPANGA KUZALISHA KUZALISHA NGUVU KAZI NCHINI



MWENYEKITI wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), Peter Maduki amesema Chuo kimejipanga kuzalisha nguvu kazi nchini,ambayo itawasaidia wawekezaji na wafanyabiashara watakaokuja nchini kufanya shughuli zao.

Maduki aliyasema hayo wakati akikagua bunifu mbalimbali katika banda la Veta ndani ya maonyesho ya 46 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba,amesema nguvukazi ya wataalamu inayozalishwa inatosha kutumika katika sekta mbalimbali kama Utalii, Viwanda, Biashara, Teknolojia, Ubunifu, Madini na Gesi.

“Mbali na nguvukazi pia tunajitahidi kuzalisha teknolojia ambazo zitatumiwa na wawekezaji ili kuhakikisha wanazalisha katika ufanisi na ubora wa kimataifa na nchi inavyotaka,”amesema na kuongeza

“Pia tunavyo vifaa vinavyotumika vinavyoweza kutumiwa na wawekezaji katika uzalishaji au kuongeza uzalishaji,” amesema Maduki

Amesema ili kufanikisha hilo pia wamejipanga kuongeza idadi ya vijana watakaopata mafunzo ya ufundi huku akieleza kuwa vyuo 29 vinamaliziwa katika ngazi ya wilaya na vinne katika ngazi ya mkoa.

“Lengo letu ni kutaka kufikia vijana 700,000 ndani ya miaka mitano wapitie katika vyuo vyetu na kujipatia ujuzi wa aina mbalimbali,” amesema Maduki.

Amesema vijana hao watapitia mfumo wa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi na kupatiwa vyeti vyao.

“Na katika hao 700,000 hatutegemei waajiriwe bali wengine wajiajiri na kuzalisha ajira pia waweze kusaidia wawekezaji watakaokuja nchini,”

Akizungumzia bunifu zinazofanywa na wanafunzi wa vyuo hivyo amesema wamekuwa wakiwasaidia wale wanaofanya vizuri kwa kiwaungajisha na Tume y Sayansi na Teknolojia (Costech) ili waweze kuendelezwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Veta Tanzania, Antony Kasore amesema wanazalisha nguvu kazi kulingana na sekta za kimkakati.

“Tunafundisha vijana namna ua kufanya kazi migodini, katika gesi ili wawezenkuwa msaada,” amesema Kasore.


Previous Post Next Post