TRA YATOA WITO KWA WATANZANIA KUTOA USHIRIKIANO WA KULIPA KODI KWA HIARI



Naibu Mkurugenzi wa Utafiti na Sera mamlaka ya mapato Tanzania TRA Ndg. Emmanuel Hezron ametoa wito kwa Watanzania kutoa ushirikiano kwa mamlaka kwa kulipa kodi kwa hiari na kuifanya TRA kuwa rafiki katika biashara zao ili kuongeza uhiari wa ulipaji kodi.

Hezron ametoa wito huo leo Alhamisi Julai 7,2022 alipotembelea banda la mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA) kujione shuguli mbalimbali zinazofanywa na watoa wa vitengo mbalimbali katika banda hilo.



Naibu Mkurugenzi huyo pia ametoa wito kwa Wanafunzi kujiunga na vilabu mbalimbali vya Kodi vilivyopo shuleni na vyuoni kwaajili ya kujenga msingi mzuri wa walipa kodi wa baadaem

Baada ya kuhutimisha ziara yake fupi katika banda la TRA amewapongeza watumishi wanaotoa huduma kwa wateja katika maoenesho ya 46 ya Biashara Sabasaba yenye kauli mbiu 'TANZANIA MAHALI SAHIHI PA BIASHARA NA UWEKEZAJI' kwenye banda la Mamlaka hiyo.

" Niwapongeze wafanyakazi wote wa mamlaka ambao wamekuwepo hapa kiukweli wanatoa huduma vizuri na kutoa maelezo yanayojitosheleza kwa watu mbalimbali wanaotembelea banda hili kwaajili ya kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya kikodi" amesema Hezron
Previous Post Next Post