Wadau wajadili mchango wa kiswahili katika ukombozi wa Afrika



Na John Mapepele


Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania leo wanashiriki kwenye kongamano la kujadili mchango wa kiswahili kuelekea siku ya kiswahili duniani hapo kesho.

 Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Dkt. Isdor Mpango ndiye anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo muhimu.



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema wakati akiongea na wageni mbalimbali leo amefafanua kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa lugha hii Serialisation imechukua wiki nzima kuadhimisha siku hii ambapo kesho ndiyo kilele chake.

Wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hili wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kukienzi kiswahili

Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Komrade Kinana amepongeza Serikali hususan uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ukiongozwa na Mhe. Mchengerwa kwa ubunifu mkubwa katika utendaji wa kazi ikiwa ni pamoja na kukitangaza kiswahili.


Mtendaji Mkuu wa Baraza la kiswahili (BAKITA) nchini, bi Consolata Mushi amesema tayari BAKITA imejiwekea mkakati mbalimbali ya kukitangaza kiswahili duniani.
Previous Post Next Post