KENYA: BASI LAPOROMOKA, 30 WAFARIKI



Takribani watu 30 wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuporomoka kwenye daraja huko Kenya. 

Basi hilo lilianguka kutoka daraja la Nithi na kuangukia kwenye mto katika mji wa Meru, kwenye barabara kuu inayotokea Nairobi. 

Afisa mmoja wa Polisi ameeleza kuwa basi hilo ambalo lilikuwa kwenye mwendo kasi litakuwa lilipatwa na shida ya kufeli kwa breki.

Previous Post Next Post