HAJI MANARA AKATAA HUKUMU YA TFF, BADO NI MSEMAJI WA YANGA



Siku kadhaa baada ya Kamati ya Maadili ya TFF kumfungia msemaji wa Yanga, Haji Manara kufungiwa kutojihusisha na soka kwa miaka 2 na faini ya Sh20 milioni kwa kukutwa na hatia ya kumtolea maneno yasiyofaa rais wa TFF, Wallace Karia leo amefunguka kwa undani sakata zima na kukataa hukumu hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo Manara amesema;

"Nakala ya hukumu sijapata, mpaka pale nitakapopata na haki ya majibu ya malalamiko yetu ya msajili na Baraza la Michezo (BMT) juu ya kutosajiliwa kanuni na mpaka pale tutakapopata haki ya kukata rufaa mimi bado Msemaji wa Yanga, hukumu haiwi hukumu mbele ya vyombo vya habari kwa mujibu wa taratibu lazima nipate nakala, sijapewa mimi bado msemaji na nitaendelea kufanya shughuli za Yanga hadi pale nipate nakala ya hukumu na kupata majibu ya BMT,"

 “Yani mimi nahusishwa mpaka na mabomu, Yani mimi nisababishe hadi mabomu ya machozi yapigwe ? RPC, Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Waziri Mkuchika wote walikuwepo pale, waniachee, mnanidhulumi ili iwe nini.

“Nimesikia ushahidi umetolewa na Katibu wa TFF ambaye anajua kila kitu anachofanya Rais wa TFF kwangu… mnanitungia mpaka mabomu? 

“Mabomu yalipigwa nje ya uwanja kwa sababu washabiki hawatoki barabarani na viongozi wa kitaifa na mkoa wanatakiwa kuingia kwenye magari yao, mechi ilikuwa imeshaisha, zawadi zimetolewa na sisi wenyewe tumeshaingia kwenye Gari tunaondoka,” Haji Manara.

Haji Manara ameeleza kuwa , lengo la kufanya mkutano na Waandishi wa habari hii leo , ni kutaka haki katika hukumu iliyotolewa dhidi yake na wala si kuomba msamaha wala kuonewa  huruma.

"Sitaki nipendelewe, sitaki nisamehewe , Isije ikaeleweka nimekuja kuomba msamaha au kutaka huruma , Sitaki huruma nataka haki itendeke" - Haji Manara 



Previous Post Next Post