SHIVYAWATA watoa mafunzo kwa waandishi wa habari kwa njia ya mtandao kwa lengo la kuwafahamisha majumumuishi ya Watu wenye ulemavu katika ajira Nchini.
Akiongoza mafunzo hapo Wakili Novatus Rukwago amesema kuwa wao kama chama wamejipanga na tayari wameshawasilima maoni yao kwa serikali kuhusu namna bora ya kuwapa fursa walemavu nchini kupata ajira katika nafasi mbalimbali nchini
"Tunapozungumzia ajira kwa watu wenye ulemavu tunajadili sambamba na Sheria zinazohusu ajira, ila muktadha huu Sheria ya watu wenye ulemavu No. 9 ya 2010" alisema Wakili Novatus Rukwago
Wakili Novatus Rukwago anaamini pia kwa kupitia vyombo vya habari watazidi kutoa elimu na kupaza sauti ili watu wenye ulemavu waweze kupata fursa ya ajira kama watu wengine