Wizara ya Maliasili na utalii kupitia bodi ya Utalii Tanzania(TTB) imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya Taifa ya vijana ya mpira wa kikapu inayoshiriki mashindano ya kimataifa nchini Uganda.
Akizungumza kwa niaba ya katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB , Felix John amesema ufadhili huo una lengo la kutangaza utalii wa Tanzania kupitia michuano ya kufuzu fainali za afrika kwa vijana chini ya miaka 18.
"TTB inajukumu la kutangaza utalii hivyo leo tumetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi 6,766,120.00 ambavyo ni pisi 24 za jezi za mpira wa kikapu rangi ya Blue , Pisi 24 za jezi za mpira wa kikapu tangi nyeusi , Pisi 35 za Traki suti juu na chini na pisi 48 za soksi" Amesema John
Umesema lengo ni kuwawezesha kushiriki ipasavyo na kushinda mashindano ikiwa na lengo la kuendeleza programu maalum ya Royal Tour ambayo imeasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Rais wa TBF Ndugu Michael Kadebe ameishukuru Wizara ya Maliasili kwa kuweza kusaidia na kuendeleza michezo nchini .
Amesema timu imeondoka na Vijana 12 wa kike na 12 wa kiume pamoja na Viongozi Makocha na Madaktari hivyo wanategemea ushindi.