TANZANIA YAWEKA HISTORIA MPYA KUPITIA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.



Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nnauye amewataka watendaji wa Shirika la Posta kuongeza wigo mpana na upanuzi wa huduma wanazozitoa kuleta tija kwa Taifa na kuongeza mapato kwa Serikali.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya kibiashara kati ya shirika la posta nchini Tanzania na Shirika la Posta  Oman ambapo amesema ushirikiano huo utasaidia kuongeza masoko baina ya mataifa hayo mawili.

Amesema kuwa, uwepo wa ushirikiano huo utazisaidia nchi zote mbili katika kuboresha huduma zitakazowalenga wananchi moja kwa moja kutoka na kodi zinazopatikana zitatekeleza miradi ya kimkakati.

"Ushirikiano huu  utaimarisha utoaji huduma inayoendana na Teknoloji ya kisasa hivyo kuimarisha shughuli za posta na kuzitambulisha, kuzitangaza huduma mbalimbali za posta Duniani kote"amesema Waziri Nape.

Ameongeza kuwa,  huduma za shirika la Posta Tanzania na Shirika la Posta la Oman yakiwemo maduka mtandao, yanaenda kuimarika zaidi kwakuwa wananchi wataagiza na kuuza bidhaa zao kwa nurahisi sana hasa kwenye biashara zinazofanyika kati ya nchi hizi mbili.

Hata hivyo, amezipongeza pande zote mbili kwa  utayari wa kushirikiana kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi lakini pia kwa kupanua wigo wa huduma wanazozitoa ndani ya nchi na nje ya mipaka ya nchi zetu.


Kwa upande wake, Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta la Oman Nasser Ahmed Nasser amesema kuwa ushirikiano huo umelenga kusaidia katika maeneo 17 ikiwemo Tanzania kuwa kitovu Cha usafirishaji wa biashara kubwa, itarahisisha kutuma pesa kutoka oman kwenda Tanzania pamoja na kuendelea na udugu uliopo.

Aidha, amesema mageuzi ya utendaji yameipa heshima Tanzania ndio maana wamekwenda kujiunga na Shirika hilo, hivyo wanaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanatoa huduma zenye kukidhi viwango na ubora.


Naye, Posta Masta Mkuu kutoka Shirika la Posta Nchini Tanzania, Macrice Mbodo amesema athakikisha wanashirikiana katika kubadilishana ujuzi na teknolojia utoaji wa huduma za posta kwa wananchi ambapo katika eneo hilo posta ya Tanzania na posta ya Oman itabadilishana ujuzi na teknolojia ya utoaji huduma za posta kwa wananchi kama vile usafirishaji wa barua, nyaraka, mizigo na sampuli za maabala, huduma za utumaji fedha na uwakala, biashara ya mtandao na huduma nyinginezo.

Aidha watashirikiana kwa kuandaa na kuchapisha stemp za pamoja za vivutio vinavyopatikana Tanzania na Oman ambazo zitauzwa Duniani kote kupitia mitandao ya uuzaji wa stemp ambapo zitatumika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana hapa tanzania na hivyo kuwavutia watalii kutoka nchi mbalimbali duniani kutembelea nchi yetu.

"Tunakwenda kushirikiana katika uunganishwaji wa maduka mtandao ambapo pamoja na kuwa litaongeza mapato kwa shirika, ushirikiano huu utawezesha watanzania kununua na kusafirishiwa bidhaa ndani na nje ya nchi zinazouzwa na kununuliwa kupitia majukwaa ya kibiashara mtandao kote duniani yatakayokuwa yameunganishwa na majukwaa mengine mtandao ya posta ya oman, tanzania na majukwaa mengine ya kimataifa"Mbodo.



Previous Post Next Post