TCRA YAZUIA KIPINDI CHA EFATHA KWA MIEZI MITATU



Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema Kituo cha Star TV kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries ambacho hurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja, kwa kuruhusu maudhui yenye ukakasi ambayo ni kinyume na Kanuni za Mawasiliano
-
TCRA ikimnukuu Askofu Josephat Mwingira imesema maneno yake kwamba "Serikali fanyeni upuuzi wenu Mungu amewaruhusu, lakini muda sio mrefu atakuja kumalizana na upumbavu wenu" yanafedhesha kutokana na Lugha isiyo na staha kwa Mamlaka ya juu ya Nchi 
-
Kipindi cha EFATHA kimesimamishwa kwa miezi mitatu, huku Star TV ikipewa onyo na kuamriwa kuomba radhi watazamaji na Umma kwa siku tatu mfululizo kuanzia Januari 25 - 27, 2022



Previous Post Next Post