Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money leo
imeutangazia umma kuwa wateja wa Airtel Money wataendelea kutuma pesa bila makato - FREE
msimu huu wa sikukuu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema,
"Kupitia huduma yetu ya Airtel Money tunaendelea kuwapa wateja wetu wote uhakika kuwa
wataendelea kufaidika na huduma ya tuma pesa popote nchini Airtel kwenda Airtel. Tuma pesa
BURE inaendelea kuwadhihirishia wateja kuwa dhamira yetu ya kuwafikishia wateja wetu
huduma zakifedha kidigitali iko palepale, huduma hii imekuja wakati muafaka kwa kuwa watu
wengi wanatuma pesa nyumbani kwaajili ya maandalizi ya shamrashamra za kusheherekea
sikukuu za chrismasi na Mwisho wa mwaka.
"Tunayo furaha kutangaza Habari Njema hii kwa wakati huu ambao huduma hii inahitajika kila
siku hasa kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za kibenki. Airtel Money inapatikana kila
kona
"Mteja anaweza kutuma kiasi chochote BURE atakachokatwa ni tozo ya serikali tu kwa mujibu
wa utaratibu wa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao lakini sisi Airtel Money hatutakuwa na
nyongeza au makato yoyote kwa mteja wetu" aliongeza Nchunda
"Airtel pia katika msimu huu tunaendelea na kupanua mtandao wetu zaidi kwa kufungua maduka
mengi zaidi ya Airtel Money Braches pamoja na huduma ya 4G nchini kote. Tunaendelea kupanua
wingo wa huduma ya 4G kwa kuongeza minara zaidi na hii itafanya mtandao wa Airtel kuendelea
kupatikana kwa urahisi na hivyo kuwafanya wateja wetu kuendelea kufurahia huduma iliyo bora
zaidi, alisema Nchunda huku akiongeza kuwa ili mteja kufurahi huduma hii kutuma pesa bure
Airtel kwenda Airtel atapiga *150*60# changua Tuma Pesa bure.
Airtel Money imekuwa ikizindua huduma na bidhaa ambazo ni zakibunifu zinazopatikana kwa
urahisi kwa kutoa huduma ya mikopo binafsi ya - Timiza Loans, mikopo ya vikundi - Timiza Vicoba
loans huku ikiwa imeunganishwa na huduma za benki zaidi ya 40 hapa nchini na hivyo kuweza
kufanya miamala kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda kwenye Airtel Money papo kwa hapo'.