Na mwandishi wetu....
Tafiti zinaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya ubunifu mpya wa teknolojia duniani unahusishwa moja kwa moja na taaluma ya uhandisi ambayo ndani yake hujumuisha masuala mbalimbali ikiwemo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Nishati, viwanda na akili mnemba.
Hayo yamebainishwa Septemba 25, 2025 jijini Dar es Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kufungua Maadhimisho ya 22 ya Siku ya Waandisi kwa Mwaka 2025.
Amesema kuwa Serikali inawahitaji na kuwategemea wahandisi nchini ambao wana fursa ya kuchangia maendeleo ya nchi kupitia utekekezaji wa majukumu yao.
Dkt. Biteko ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya uvumbuzi na maendeleo ya viwanda huhitaji huduma ya wahandisi moja kwa moja.
“ Kwa niaba ya Serikali naomba niwakumbushe kuwa taifa linawategemea sana. Tunawategemea, tunawahitaji naomba mjue Serikali itaendelea kuwategemea wakati wote mnapotekeleza majukumu yenu,” amesema Dkt. Biteko.
Aidha, Dkt. Biteko ameitaka ERB kuwasaidia wahandisi nchini kwa kuwaelekeza na kuwapa motisha pale wanapofanya vizuri badala ya kubaki kuwa tishio kwao na kuwapa adhabu baada ya kukosea.
Ameendelea kusema motisha kwa wahandisi wazawa walioshiriki katika ujenzi wa miradi ya kimkakati nchini sambamba na kuwapa hamasa na kuwajengea uwezo wa kushiriki miradi mingine ya kimkakati ni muhimu ili kuwapata wahandisi wazalendo
Naye, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa Wizara itaendelea kuimarisha mazingira ya taaluma ya uhandisi ikiwa ni pamoja na kuruhusu mafunzo ya kuongeza viwango vya taaluma hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Menye Manga amesema katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imetekeleza miradi mikubwa ikiwemo
daraja la Kigongo Busis na wahandisi wengi wa wazawa wameshiriki katika kujenga tofauti na ilivyokuwa awali.