Na mwandishi wetu...
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (THTU), Ndugu Kailima R.K (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Ofisi ya Tume Zanzibar, Ndugu Adam Mkina, wakishuhudia ubandikaji wa fomu za uteuzi za Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Mhe. Luhaga Joelson Mpina, pamoja na Mgombea Mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej.
Zoezi hilo limefanyika leo, tarehe 13 Septemba 2025, majira ya saa 10:00 jioni, ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya kisheria yanayowataka wagombea kubandika fomu za uteuzi kwa muda wa saa 24. Lengo ni kutoa fursa kwa mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasilisha pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea husika, endapo kutakuwa na sababu za msingi.