Na mwandishi weru
Ipo taarifa ya upotoshaji na uongo inayosambaa katika mitandao ya
kijamii inayoeleza kwamba, mfumo wa Data za uchaguzi unaotumiwa
na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi umeunganishwa na mfumo wa
NIDA na Chama kimoja cha Siasa na kwamba zoezi la upigaji kura(uchaguzi) limeshamalizwa.
Napenda kutoa taarifa kwamba, Taarifa hiyo siyo sahihi, ni upotoshwaji
na uongo kwa sababu zifuatazo:
(i) Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye
hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi.
(ii) Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo
wowote wa Serikali au wa Taasisi binafsi kwa madhumuni ya
upigaji kura.
(iii) Mfumo wa upigaji wa kura, kuhesabukura na kutangaza matokeo
hautumii mfumo wa aina yoyote wa kielekroniki.
(iv) Mfumo wa upigaji kura, kuhesabu kura na kutanza matokeo
hutumia utaratibu wa kawaida (manual).
(v) Baada ya kukamilika kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari, vyama
vya siasa vilikabidhiwa Daftari husika linaloonesha idadi ya
wapiga kura walioandikishwa katika kila kituo.
(vi) Mawakala wa upigaji kura kutoka kwenye vyama vya siasa
vinavyoshiriki uchaguzi hutumia Daftari husika kuwezakumtambua mpiga kura anayefika kituo kwa ajili ya kupiga kura.
(vii) Mfumo wa upigaji kura kwa Tanzania, mtu aliyeandikishwa hufika
mwenyewe katika kituo cha kupigia kura na kuonesha kadi yakeya mpiga kura iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,ambapo jina lake husomwa kwa sauti na msimamizi wa kituo ili
kuwawezesha mawakala wa upigaji kura kujiridhisha iwapo mtuhuyo yupo katika Daftari walilopewa, baada ya uhakiki huo ndipomhusika hupewa karatasi za kura ili aendelee na utaratibu wakupiga kura, na
(viii) Ifahamike kuwa, Kitambulisho cha Taifa hakitumiki kupigia kura,
bali Kadi ya mpiga kura pekee iliyotolewa na Tume Huru ya Taifaya Uchaguzi na kuhakikiwa ndiyo inayotumika wakati wa upigajikura katika vituo vya kupigia kura.
Tume inawasihi wananchi na wadau wote wa uchaguzi kuupuza uongona upotoshaji huo, na anayesambaza ana lengo la kuzua taharuki naupuuzwe kama wapotoshaji wengine.
Aidha, katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika tarehe 29 Oktoba, 2025, taarifa zote sahihi kuhusu Tumezitapatikana kwenye vyanzo rasmi ikiwa ni pamoja na tovuti ya Tume(www.inec.go.tz) na kurasa za Tume kwenye mitandao ya kijamii.
"KURA YAKO HAKI YAKO JITOKEZE KUPIGA KURA"
Imetolewa leo tarehe 23 Agosti 2025; nay
Kailima, R. K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI2


