Na Lilian Ekonga.....
Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata huduma ya msaada wa kisheria bila kujali wapi alipo, Asasi isiyo ya Kiserikali ya Legal Services Facility (LSF) kwa kushirikiana na kampuni ya kiteknolojia ya TechForward wamezindua rasmi mtandao wa kidigitali wa msaada wa kisheria unaoitwa 'HAKI YANGU' chat bot.
Akizungumza katika hafla uzinduzi Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Bi. Lulu Ng’wanakilala, amesema Mfumo huo unaendeshwa kwa akili Bandia AI ikibuniwa mahususi kusaidia wasaidizi wa kisheria na wananchi kupata huduma za msaada wa kisheria kwa wakati,usahihi na usalama.
"Kupitia jukwaa hili wasaidizi wa kisheria watakuwa na ufikiaji wa taarifa sahihi za kisheria kwa masaa 24 siku yoyote popote pale walipo, wananchi wataweza kuwasiliana na mfumo wenye akili bandia unaoelewa maswali yao ya kisheria na kuwaunganisha na njia za rufaa pale ambapo kesi inazidi uwezo wa mtoa huduma za msaada wa kisheria.
Ameongeza kuwa Mfumo huo umejengewa maudhui ya kisheria yaliyohakikiwa na njia za msaada na kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma hususani wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na jamii ambazo hazipati huduma zinazohitaji.
Kwa upande wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA (ICT Commission), Dkt. Nkundwe Mwasaga, alieleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya usambazaji wa mtandao katika maeneo ya vijijini ili kuhakikisha huduma kama hizi zinamfikia kila Mtanzania.
" Serikali inajenga minara zaid ya 750 ili huduma ziwafikie watu wengi ambapo itasidia huduma iweze kuwafikia watu wengi zaidi ambapo idadi ya simu janja inakuwa zaidi kutoka na takwimu ya TCRA inasema simu janja zipo milioni 24" amesema Mwasanga.
Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa TechForward, Bw. Elias Patric, amesema 'HAKI YANGU' chat bot inakipengele kinachomuwezeaha mtumiaji kuunganishwa na mtoa huduma za msaada wa kisheria aliyekaribu kili kupata msaada wa kisheria bila malipo karibu na anapoishi.
"Programu hiyo inapatikana kupitia simu janja au kompyuta, na inatoa huduma kwa lugha rahisi na rafiki kwa mtumiaji ya kiswahili Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa kila mmoja, hususan wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, wanaweza kufikia haki bila vikwazo" amesema





