TANZANIA MWENYEJI WA KONGAMANO LA 18 LA KIMATAIFA LA e LEARNING AFRIKA




Na Lilian Ekonga......

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Kongamano la 18 la kimataifa la e Learning Afrika ambalo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili utekelezaji wa ajenda ya kuimarsiaha ukuaji wa Sekta ya elimu Barani Afrika kwa njia ya kidigitali ili kuendana na

Akitoa Taarifa hiyo iliyolenga kuelezea Kongamano hilo litakalo fanyika Mei 7 hadi 9 Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia  Prof. Ladislaus Mnyone amesema kufanyika kwa Kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya kukuza Sekta ya elimu katika Bara la Afrika.

Amesema kongamano hilo linatarajiwa kukutanisha mawaziri 20 na Viongozi mbalimbali kutoka Bara la Afrika pamoja na Washiriki takribani 1300 huku watanzania wakiwa 500.

"Lengo la kuongamano hili ni kuleta wadau kutoka kwenye makundi mbalimbali ikiwemo Wataalamu,Wafanayabisahara, Wawekezaji, Watafiti, Wabunifu kwajili ya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja kama Bara la Afrika ya namna gani tutachagiza maendeleo ya matumizi ya tekenolojia ya kidigital kwenye ya Elimu" amesema Mnyone


Ameongeza kuwa Kauli mbiu ya Kongamono hilo ni Kufikiria upya Elimu na Rasimali watu kwaaajili ya Ustawi wa Afrika huku mada mbalimbali kizijadiliwa katika maeneo tofauto na kuona kwa namna gani Elimu itaweza kuzalisha zaidi rasimali watu na kuongeza maendeleo na matumizi ya kidigitali.

"Kwenye kongamano hili kutoka na mijadala kuhusu maswala ya teknolojia za kidigital, Mikutano ya Mashirikano na kutengeneza mashirikiano baina ya nchi na nchi,Mashirika na Makampuni binafsi, Pia kutakuwa na mkutano wa Mawaziri" amesema





Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tehama Wizara ya elimu,Lina Rujweka ameseme kwenye kongamano hilo wamealika wabunifu mbalimbali ambao wanataonyesha bunifu zao ambazo zitasidia katika sekta ya Elimu

"Tumealika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Tamisemi, Mamlaka ya serikali Mtandao, Wizara ya AFya na Wizara ya Fedha hawa wote watakuja kuonyesha teknolojia Bunifu ambazo tunazo" amesema Rejweka

Nae Samson Sitta,Afisa Programu Milele Zanzibar Foundation amesema wamesikia fahari sana kujumika kwa kwenye kongamana la e learninga kwa lengo kujifunza kwenye mataifa mbalimbali na kuonyesha ubunifu mbalimbali ambao tanzania tumeweza kubuni
Previous Post Next Post