WASHINDI TUZO YA UANDISHI BUNIFU YA MWALIMU NYERERE








Washindi wa kwanza wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2025 kutoka vipengele vinne ambavyo ni Ushairi, Riwaya, Tamthilia na Vitabu vya Watoto wamepokea mfano wa hundi ya Shilingi Milioni kumi kwa kila mmoja.

Washindi hao wamekabidhiwa Mfano wa hundi hizo pamoja na Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambapo Tuzo hizo zimekabidhiwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mhe Dkt Philip Mpango.

Hafla ya utoaji Tuzo hizo imefanyika mnamo Aprili 13, 2025 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa the Super Dome Masaki ambapo viongozi mbalimbali na watu mashuhuri walihudhuria usiku wa Tuzo hizo akiwemo Mgeni maalum Prof. Ibrahim Noor ambaye ni Mhadhiri, Mwandishi wa vitabu na Mchoraji Maarufu kutoka Chuo Kikuu cha Sultan Quaboos kilichopo Nchini Oman.



Previous Post Next Post