NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA VITAMBULISHO KWA WASIOFUATA MEI 1






MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa, (NIDA) imesema itasitisha matumizi ya namba za vitambulisho vya NIDA kuanzia Mei 1, mwaka huu, kwa wananchi wote waliotumiwa jumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa ajili ya kwenda kuchukua vitambulisho vyao na hawajavifuata.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 14, 2025 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu
wa NIDA, James Kaji alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

“Niwazi NIDA imesikitishwa na idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza kuchukua vitambulisho vyao tumekuwa tukituma ujumbe mfupi kwa wananchi kuwaelekeza ni mahali gani waende kuchukua vitambulisho vyao lakini idadi ni ndogo sana hivyo basi NIDA tumeamua kuwa tutasitisha matumizi ya namba za vitambulisho, kwa wale wote ambao wameshatumiwa jumbe za kuchukua vitambulisho lakini hawajachukua,” amesema Kaji.


Ameongeza: “Niseme tu kwamba tangu kuanza kwa zoezi la kukusanya vitambulisho na
kutuma sms mwezi Januari,mwaka huu mpaka kufikia Machi 23, 2025, jumla ya wananchi 1, 880, 608 sawa na asilimia 157 ya watu wote waliokuwa hawajachukua vitambulisho vyao,idadi ya wananchi waliojitokeza kuchukua
vitambulisho baada ya kupokea sms ni 565,876 sawa na asilimia 30,”amesema Kaji.

Amesema kuanzia sasa mtu anaposajiliwa itachukua siku tano mlengwa kupokea ujumbe wa namba yake ya NIDA na ndani ya siku 21 atapokea ujumbe kuwa akachukue kitambulisho kikotayari katika ofisi fulani na mwezi mmoja utatolewa na asipoenda kuchukua kitambulisho hicho kitafutwa na kusisitiza mtu anapopata ujumbe wa kwenda kufata kitambulisho ahakikishe anatunza ujumbe huo ili aweze kwenda nao kwenye ofisi za NIDA ili kuepusha usumbufu.


Amesema katika kutekeleza maagizo ya Rais Samia NIDA imeandaa mpango wa usajili na utambuzi wa watu wote wenye umri chini ya miaka 18 kwa kuwezesha
upatikanaji wa jamii namba pamoja na kundi hilo na kwa wageni wote wanaoingia nchini na kukaa chini ya miezi sita.

“Kwa sasa wageni wanaosajliwa, kutambuliwa na kupewa jamii namba ni wale wanaokaa nchini kwa zaidi ya miezi sita na wenye kibali cha makazi.Mpango huu wa usajili wa watu wenye umri chini ya miaka 18 utaanza kwa majaribio (pilot) katika wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Kusini-Kusini
Unguja, Kilolo – Iringa na Rungwe – Mbeya ambapo tunatarajia kusajili
jumla ya watu 235,826 ndani ya miezi miwili,”amesema Kaji.

Amesema NIDA inafikiria kuwepo kwa faini kwa wale wasiozingatia jambo hilo hili hali serikali inatumia fedha nyingi kuhakikisha kila mmoja anapata kitambulisho bila gharama yeyote.

Kaji ametoa rai kwa kila mtu aliyekwisha fikisha miaka 18 kwenda kujiandikisha ilikupata kitambulisho hicho na si kusubiri wakati wa shida.
“Tumekuwa tukipata changamoto kubwa wakati ajira zinapotolewa kwani vijana wengi huja kwa wingi ofisini kwetu kuomba kitambulisho kwa wakati huo na kutoa maneno machafu kwa wafanyakazi wetu,nitoe rai kwao wanapotimiza miaka 18 wahakikishe wanajiandikisha kwa wakati pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa wahudumu ilikuepusha usumbufu pale ajira zinapotolewa,”amesema Kaji.

Amesema NIDA inaendelea kufaya maboresho ya mifumo kwa kuwaamisha wadau kutoka mfumo wa awali na kuja katika mifumo mipya itakayomuwezesha mwananchi kuzikubali taarifa zake pamoja na utunzaji wa taarifa hizo kwani NIDA ndiyo kila kitu baada ya kuwa mtu kaweka dole gumba.

Kaji ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandio ya kijamii kuhusu NIDA
 kusajili bima ya toto afya kadi kuwa taarifa hiyo si kweli na kama Mamlaka haina usijali wowote

Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo ilipokea maelekezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamana kuwa kila sehemu palipo na ofisi ya NIDA lazima Ofisa uhamiaji awepo ili kuepusha usumbufu kwa wananchi kwenda kumtafuta na kuwasaidia,suala hilo limefanyiwa kazi.

Kaji amesema tatizo la vitambulisho kufutika limekwisha fanyiwa kazi kupitia mwanasheria mkuu wa serikali na tayari wengine wamekwisha anza kupewa vipya na kutoa rai kwa wananchi kujaza fomu kwa usahihi ilikuepusha changamoto ya kukosewa kwa majina.
Previous Post Next Post