MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA HESLB, RAIS MWINYI AELEKEZA KUONGEZWA VYUO VYA ELIMU YA JUU ZANZIBAR



Na Lilian Ekonga

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuelekeza Waziri wa Elimu sayansi na teknolojia Dkt. Aldof Mkenda kuendelea kutafuta fursa ya kuongeza vyuo na kampus ya vyuo vikuu vingi zaidi Zanzibar vitakavyokidhi mahitaji ya vijana ili kuendelea kuimarisha muungano wetu katika nanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi kupitia uwezeshaji wa elimu ya juu.

Ameyasema yao leo februari 15, Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hamza Hassan Juma wakati akisoma hotuba ya Rais wa zanzibar Dkt. Hussen Ali Mwinyi katika maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya mikopo ya elimu ya juu HESLB iliyoambatana na mbio za hisani yenye lengo la kukusanya fedha kwajili kuboresha miundombinu ya shule mbili zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.

Pia amezipongeza taasisi zetu zote za elimu ambazo tayari zimetumia fursa ya kuanzisha kampusi na matawi yao zanzibar jambo ambalo linaweza kupanua wigo na fursa ya kuimarisha daraja la muungano kwa faida na wananchi wa pande zote mbili.


"Takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2004 hadi 2025 takribani watanzania laki 8 wamegaramiwa masoma yao ta elimu ya juu katika fani mbalimbali hii ni ishara njema na dhamira ya dhati ya serikali katika kuwezesha vijana wa kitanzania kufika ndoto zao za kupata elimu ya juu" amesema juma

Ameongeza kuwa kuwepo kwa mikopo ya elimu juu kumewezesha watoto wengi wenye uhitaji na wanaotoka katika kaya masikini kufikia ndoto za maisha yao.

Aidha amesema kwa upande wa zanzibar pia kuna Bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo imetoa mchango mkubwa kws vijana wetu, lakini hii ya muungano imetoa mchango mkubwa kwa wanafunzi wengi zaidi.

"Mafanikio haya ya bodi ni fursa muhimu ya kutasimini mafanikio yote yaliyopatikana na kupanga kwaajili ta mafanikio makubwa zaidi katika siku za mbele zijazo" ameongeza juma





Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipanga amesema kuwa mwaka 2021/22 wakati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu ilikua shilingi bilioni 464,ambapo ndani ya miaka minne ya uongozi wake imepanda hadi kufikia shilingi bilioni 787.

"Kwa kipekee mheshimiwa mgeni rasmi tufikishie salamu zetu kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Mwinyi kwa kazi hii kubwa ya kupandisha bajeti ya Bodi ya Mikopo kwa zaidi ya asilimia 90,sisi kama Wizara tunajivunia,lakini tunashukuru viongozi wetu kwa utashi wao wa kisiasa kwa kuona eneo hili la Elimu ni eneo muhimu sana" amesema Mh. Kipanga


Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu HESLB, Dkt Bill Kiwia amesema bodi ya mikopi ilianza na wanafunzi elfu 48 na ilikuwa na bajeti ya milioni 53.1 na hadi kufikia mwaka 2024, 25 wametoa jumla.ya bilioni 787 kwa ajili ya wanafun zi zaid ya laki 2,457,99

"Jumla ya mikopo ambayo tumeshatoa tangu kuanzishwa mapaka sasa ni trilioni 8.2 ambayo imeweza kusomesha wanafunzi laki 8,30000 nchi nzima" amesema Kiwia




Aidha ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya rais samia Suluhu Hassan kwa kipinidi cha serikali yake wametoa zaid ya trilion 2.7 kwaajili ya kusomesha vijana.

"Mbio hizi zinalenga kukusanya milioni 100 katika kuboresha miundombinu na mifumo ya shule za sekondari kwa kukarabati shule mbili za sekondari moja tanzania bara na zanzibar ambapo makusanyo ya mbio hizo wataenda kuboresha shule hizo kama sehem ya mchango katika katika maendeleo ya Elimu" amesema kiwia






Previous Post Next Post