Na Lilian Ekonga........
Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) imeendelea kuimarisha huduma zake za kibenki kidigital nchini kwa kuwazawadia wateja wake wanaofanya miamala kwa njia za kidigitali kupitia kampeni ya Mahaba Kisiwani
Kampeni hiyo imewazawadia wateja waliofanya miamala mingi katika msimu wa wapendanao wakigharamiwa safari ya kwenda Zanzibar na malazi wawapo visiwani humo.
Ameyasema hayo leo februari 14 jijini Dar -es salaam, Mkurugenzi wa biashara na wateja wadogo, Lilian Mtali akimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa TCB, Adam Mihayo katika hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya huduma na ubora wa benki ya tangu kuanzishwa kwake sambamba na kutoa zawadi kwa washindi wa kampeni ya mahaba kisiwani.
Mtali amesema Kampeni ya Mahaba Kisiwani inadhihirisha malengo ya kimkakati ya TCB kutumia teknolojia kukuza matumizi ya njia za kidijitali katika kufanya malipo.
"Kwa kuwazawadia wateja, Benki ya TCB inapanua wigo wakutoa huduma za kibenki kwa wateja wake kupitia njia mbalimbali, pamoja na kuwapa hamasa wateja kutumia njia hizi zilizo salama zaidi, zenye ufanisi, na rafiki kwao" amesema Mtali
Ameongeza kuwa Kampeni Mahaba Kisiwani ilibuniwa ili kuwahimiza wateja wao kufanya miamala kidijitali huku wakijiongezea nafasi ya kushinda safari ya kwenda wikiendi kisiwani Zanzibar.
Alikadhalika amesema “Mafanikio ya benki yetu katika kipindi cha miaka 100 iliyopita ni matokeo ya juhudi na bidii za kila mmojawetu.Tunadhamiria kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ambayo kila mmoja anathaminiwa, anaungwa mkono na kuwezeshwa tunapoendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu.
Mchango wa kila mmoja wetu ndio sababu leo tumefika hapa, nina imani tutaendelea kuimarika, na kuweka mfano wa kuigwa wa huduma bora na uvumbuzi katika siku za usoni,” aliongeza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha kidijitaji na Ubunifu, Jesse Jackson amewasihi watu wote kuendelea kutumia huduma zai za kidigitali kwa kufanya miamala mbalimbali kwani inawarahisishia kupata huduma kwa haraka zaidi bila hata kufika kwenye tawi ya benki hiyo