Na mwandishi wetu............
KATIKA kuendelea kutatua changamoto zinazowakumba wanawake nchini,Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Her Initiative kupita jukwaa la panda Digital limetambulisha huduma ya Panda chat ambalo ni jukwaa litakalotumika kuwasaidia wajasirimali wasichana kuripoti changamoto zinazowakabili.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati uzinduzi wa Panda Chart,Mkurugenzi Mtendaji wa Her Intiative,Lydia Charles Moyo,amesema jukwaa hilo litaleta suluhisho kwa changamoto zinazowakumba wanawake na kuweza kupatiwa suluhisho.
"Wasichana wenge wajasiriamali hukumbana na changamoto mbalimbali,zikiwemo upungufu wa maarifa ya kitaalamu katika kuendesha biashara,ukosefu wa mitandao ya msaada wa kibiashara,changamoto za kijami kama ukatili wa kijinsia na Rushwa ya ngono zinazozuia maendeleo yao ,na kukosa Rasilimali za kuhimili ushindani wa kibiashara "Amesema Moyo.
AMeongeza kuwa kupitia jukwaa la Panda chat litaleta suluhisho kwa changamoto hizo kwa kuwapa wajasiriamali fursa za kujifunza kutoka kwa wataalamu wa sekta mbalimbali za biashara,kubadilishana mawazo na wajasiriamali wenzao,na kupata mwongozo wa kitaalamu kuhusu changamoto za masoko,usimamizi wa fedha,na kupata mwongozo wa kitaalamu kuhusu changamoto za masoko,usimamizi wa fedha,na mbinu za kuvutia wateja.
"Elimu pekee haitoshi kuondoa changamoto zinazokuwakumba wajasiriamali wanawake.Tunahitaji kuweka mazingira yanayowawezesha kwa kuwapa msaada wa kiufundi na kitaalamu kwa kuwakutanisha wabobezi wa masuala ya kiashara haswa katika ulimwengu huu wa kidigitali"Amesema .
Hata hivyo lydia ,amesema Panda Chat inakuja kama sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya Haki haiuzwi kwa mwaka 2024-2025,kampeni ya Haki Haiuzwi inalenga kutengeneza vinara wa kupinga Rushwa ya ngono miongoni mwa wasichana wajasiriamali,na imejikita kutoa ujasiri na maarifa ya kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa upande wake Diana Joseph ambaye ni kinara wa kampeni ya Haki haiuzwi, amesema wasichana wengi wamekuwa wakipitia changamoto za nyingi sana katika maeneo yao ya kazi hasa Rushwa ya ngono katika harakati zao za kazi, ndomana wakaja na kampeni hii ya ili kupaza sauti ya wahanga wote waliokutana na changamoto kama hizo ikiwemo kutoa elimu kwa vijana wote wakike na wakiume ili kukomesha hali hiyo na kuweka usawa katika nyanja zote za kiuchumi
"Tumelenga kutoa elimu hii vyuoni na masokoni kwa wafanyabiashara wote na tunatarajia kuanza katika soko la mwananyamala kisha tutaendelea na maeneo mengine zaidi ili kuhakikisha elimu hii inawafikia watu wengi zaidi hasa vijana wakike na wanawake ambao ndo wahanga wa kubwa katika chamgamoto hiui" amesema Diana.
Nae Leticia Samson ambae ni kinara wa kampeni ya Haki haiuzwi amesema navijunia kushiriki kwenye kampeni itayaweza kuwasaidi watu kusema changamoto zao za rushwa ya Ngono na pia jukwaa la ongea hub litakuwa ni rafiki kwa watanzania kwakuwa lugha itakayo inatumika ni lugha ya kiswahili.