WANAFUNZI 974,332 WACHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2025





Na Mwandishi wetu.......


Zaidi ya wanafunzi Laki Tisa waliohitimu Elimu ya msingi mwaka 2024 wamepangiwa Shule za Sekondari kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza mwezi Januari mwaka 2025.

Idadi hiyo imetangazwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwawakati akizungumza na waandishi ws habari, huku akisisitiza kuwa kati ya wanafunzi hao, Wanawake ni zaidi ya Laki Tano na wanaume ni zaidi ya Laki Nne.

Waziri Mchengerwa, ametangaza idadi ya wananfunzi hao waliopangiwa Shule za Sekondari za serikali, akisema idadi hiyo ni saw ana asilimia 100.

Aidha, mahitaji maalumu waliochaguluwa ni 3,067 wasichana wakiwa 1,402 na wavulana 1,665.

Waziri Mchengerwa, amesema wanafunzi wote waliochaguliwa kwa mwaka wa masomo 2025, wanatakiwa kuanza masomo Januari 13 mwakani.
Pamoja na hayo, amewataka wazazi na walezi kufanya maandalizi mapema kwa watoto wao ili kuepuka watoto kuchelewa kuanza masomo kwa wakati.


Previous Post Next Post