TRA KUENDELEA KUWA NA VIKAO VYA MARA KWA MARA NA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZAO







Na Lilian Ekonga.........

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ,Yusuph Juma Mwenda ameitaka Ofisi ya Mkoa wa Kikodi wa TRA iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam kuendeleza vikao vya mara kwa mara kati yake pamoja na Jumuiya ya wafanyabishara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo ili kuendelea kuzifanyia kazi Changamoto na kero zinazo wakabili wafanyabishara hao.

Ameyasema hayo leo Disemba 20 jijini Dar es salaam. wakati alipotembelea ofisi ya TRA mkoa wa kikodi na maduka ya baadhi ya wafanyabiashara kwa lengo la kuwashukuru na kwa ushirikiano wao mzuri wa ulipaji kodi


"Nataka niwahakikishie kuwa, kwa kasi hiyo ya utatuzi wa changamoto hizo za kisera na kiutawala, kwa nchi zote zinazotuzunguka katika ukanda wa Afrika tunataka zije Kariakoo kufanya biashara na nyie na huo ndio msimamo wetu,”amesema






Aliongeza kuwa, TRA, inamaslai na Kariakoo ikiwa inafanyabiashara kubwa, kwani wafanyabiashara watapata faida hivyo na serikali kukusanya kodi. 

Alieleza kuwa, katika kurahisisha shughuli za wafanyabiashara wa Kariakoo wameendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili huku wakitenga siku moja kila wiki ya kukutana na wafanyabiashara hao kuzungumza nao.

Mwenda amesema kwa maagizo hayo aliyoyatoa kwa viongozi wa Mkoa wa Kikodi Kariakoo, wamekuwa wakitekeleza agizo hilo kwa mafanikio makubwa ya kuendelea kutatua changamoto zao.

“Nawashukuru sana wafanyabiashara wa kariakoo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano, kukaa vikao  kutatua changamoto na kukubaliana, kwani tangu nianze kazi yangu kama kamishna Mwezi Julai, upo ushirikiano mzuri kati ya wafanyabishara wa kariakoo na watu wa TRA Kariakoo, nawapongeza sana,”amesema 

Aliwashukuru wafanyabiashara wa Kariakoo kwa kulipa kodi kwa hiari yao kuwezesha Mkoa wa Kikodi Kariakoo, kuvuka lengo lililokuwa limekusudiwa na kufikia asilimia 108.




Amesema TRA ni sehemu ya wafanyabiashara, hivyo viongozi wanaowachagua watahakikisha wanashirikiana nao, kufanya kazi nao, hivyo viongozi wanaochaguliwa  wanawatambua na kushirikiana nao.

Kuhusu changamoto zilizopo za machinga, wanaokwepa kodi na wale wanaokiuka utaratibu watahakikisha zinatatuliwa kuhakikisha biashara zinafanyika vizuri ikiwa ndiyo msimamo wao.

Vilevile alisema wapo wafanyabishara wanao fanya mauzo hewa kwa kuonyesha risiti za mauzo kubwa na za kughushi kwa lengo la kupunguza malipo ya kodi yanayotakiwa.

Aliwasisitiza wafanyabiashara kuacha utaratibu huo, kwani wanatambua wote wanaofanya hivyo na watawachukulia hatu kali wote wanaohusika, hivyo wasipoacha wakibainika watalipa faini na kodi zote walizokwepa.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani, Ted Frank, alimpongeza Kamishna Mwenda huku akisema kuwa wataendelea kusimamia na kutekeleza miongozo yote anayoitoa.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa TRA, Moshi Kabengwe, alisema wanaendelea kuimarisha ushirikiano na wafanyabiashara na walipa kodi mbalimbali kuhakikisha kuwa wanalipa kodi kwa hiari na kutambua umuhimu wake.

Nae Peter joseph mfanya biashara  kariakoo amewapongeza ma ofisa wa TRA wote kwa kufanya kazi wa weledi na wafanya biashara wa kariakoo

"Sisi wafanyabiashara wale mstari ws mbele kulipa kodi, kwa kuzingizatia taratibu za kikodi ili uweze kulipa kodi, bila kusukumwa sisi wafanyabiashara wakubwa ns wadogo tulipe kodi ilu tujenge taifa letu na kuisaidia serikali" amesema Joseph.

Bashiru Mohhamed mfanyabiashara  kariakoo amesema amewapongeza  TRA kwakuwa waelewa na kuendeleza semina wanzofanya kila alhamisi kwa wafanyabiashara






Previous Post Next Post