Na Mwandishi wetu........
.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya uchukuzi ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya Uchukuzi kwa lengo la kuwatambua na kuwasajili wana taaluma hao
Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 20,2024 na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile katika mahafali ya 40 ya Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),amesema bodi hiyo pia itakuwa na jukumu la kusimamia weledi na maadili ya watalaam wa uchukuzi Tanzania Bara.
Amesema uanzishwaji wa bodi hiyo una lengo la kuhakikisha kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki.
Akizungumzia kuhusu NIT,Kihenzile amesema serikali itaendelea kukiwezesha chuo cha NIT kwa kukiboreshea miundombinu yake ya kufundishia ili kuhakikisha kinatimiza majukumu yake ya kuandaa wataalam, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu katika sekta ya uchukuzi kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu.
Kihenzile ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa usafiri na usafirishaji kuunga mkono jitihada za Chuo katika kuwapatia nafasi za mafunzo kwa vitendo wanafunzi na kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni ili zitumike kwa maendeleo ya nchi.
Aidha ametoa rai kwa wadau na wafaidika wa shughuli za chuo na taasisi za umma na binafsi kuunga mkono jitihada za chuo hizo katika kupata nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni ili ziweze kutumi kwa maendeleo ya nchi.
"Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo NIT ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya usajili wa wataalam wa uchukuzi lengo likiwa ni kuwa tambua , kuwasajilu na kusimamka weledi wa maadili ya wataalam wa uchukuzi Tanzania Bara ili kuhakikisha kwamba kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki" amesema naib Waziri.
Awali Mkuu wa chuo cha NIT, Mhandisi Dkt Prosper Mgaya amesema katika mahafali hayo wahitimu 4,176 wametunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali kati yao wanaume ni 2,581 na wanawake 1,595.
Akizungumzia changamoto amesema chuo kimekuwa na mikakati ya kukabiliana nazo zikiwemo za miundombinu na upungufu wa rasilimali watu sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwa kuweka mikakati mbalimbali.
Amesema sambamba na mabweni chuo kinajenga ofisi,madarasa na karakana ambapo jumla ya majengo matatu yanajengwa na yanatarajiwa kukamilika Februari 2025 ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa EASTRIP.
Amesema chuo pia kinaanzisha kampasi mpya mkoani Lindi na Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kampasi ya Dar es Salaam na kuhusu rasilimali watu ili kukabiliana nalo wanaendelea kuomba vibali vya ajira Serikalini ili kupunguza matumizi ya wahadhili wa muda.