NABII MALISA ATABIRI MAMBO MAKUBWA KUELEKEA MWAKA 2025



Na Mwandishi wetu.......


Nabii Clear Malisa wa Kanisa la Madhabahu ya Hatma ametabiri kwamba mwaka 2025 dunia itarudi katika kipindi cha miaka 1950 iliyopita, ambapo mifumo ya mawasiliano na intaneti itakatika na mifumo ya kibenki itasimama.

Alikalika Ametoa wito kwa serikali kuchukua hatua mapema na jamii kujiandaa kifikra, ikiwemo kuweka mikakati ya kukabiliana na uhalifu unaoweza kutokea.


Malisa ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuzungumzia mkesha mkubwa unaotarajia kufanyika leo kanisani hapo Ubungo Jijini hapa.

"Rais Samia amekuwa na ushirikiano mkubwa kwetu viongozi wa dini,tunamshukuru kutobagua dhehebu lolote"Amesema Malisa.

Hata hivyo,Malisa ameutabiri mwaka 2025 utakuwa mwaka wa neema zaidi kwa Taifa la Tanzania katika nyanja ya uchumi ikiwemo kupanda kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola za Kimarekani.

Akizungumzia suala la Utabiri anaofanya,kiongozi huyo kwa kiroho amesema ni Utashi ambao Mungu amempa na kuhaidi kutoa utabiri juu ya mambo mbalimbali kuhusu uchaguzi mkuu wa hapo mwakani kupitia kwenye mkesha utakaofanyika kanisani hapo.

Sanjari na hayo,Malisa ametumia mkutano huo kuwataka watanzania kipindi hiki cha mkesha huu wa mwisho wa mwaka kujitokeza kwenye nyumba za Ibada kufanya maombi na kumshukuru Mungu.
Aidha, Nabii Malisa amebashiri kuwa uchumi wa Tanzania utaimarika mwaka 2025, na shilingi ya Tanzania itapanda na kuwa juu, ikipiku Dola ya Kimarekani. Vilevile, ametabiri kuwa magonjwa ya Kansa na HIV yatapata tiba duniani kote, huku jamii ikishauriwa kuchukua tahadhari na kujiandaa kwa mabadiliko haya makubwa.
Previous Post Next Post