Na Mwandishi wetu Geita
Kesi namba No. 32126/2024 inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Msingi Waja Josphat masenema anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake imeendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita.
Kesi hiyo ambayo imetajwa Mahakamani Desemba 12, 2024, mbele ya Hakimu Mkazi Geita, Cleofas Waane, mashahidi watatu upande wa Jamhuri wametoa ushahidi wao, wakiongozwa na Wakili wa Serikali Verena Mathias.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Jumatatu Desemba 16, 2024 ambapo itaendelea katika hatua za kusikiliza ushahidi.
Itakumbukwa mtuhumiwa alifikishwa mahakamani siku chache baada ya familia ya mtoto anayedaiwa kufanyiwa ukatili huo pamoja na wadau kupaza sauti kutaka mtuhumiwa afikishwe mahakamani, kutokana na kudai uwepo wa 'mazingira yenye mashaka ya haki kutendeka'.
Chanzo Mwanahalisi Digital..