MAJALIWA MGENI RASMI KONGAMANO LA 14 LA IET








Na Lilian Ekonga....


Taasisi ya wahandisi Tanzania (IET) kwa kushirikian na Bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) imeandaa kongamano la kimataifa la 14 ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji ya Taasisi ya Wahandisi Tanzania(IET),Ipyana Moses amesema kongamano hilo linatrajiwa kufanyika tarehe 4 Desemba mpaka tarehe 6 Desemba mwaka huu kwenye ukumbi wa kimataifa Arusha(AICC) jijini Arusha

Amesema katika kongamano hilo wanatazamia wahandisi, mafundi , wanafunzi na wadau wengine kutoka mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi kushiriki.

Pia amesema wapo ambao watashiriki kwa niia ya mtandao ambapo jumla ta washiriki wanatarajiwa kuwa zaidi ya elfu moja .

Aidha amesema katika kongamano hilo kutakuwa na mawasilisho ya mada mbalimbali ambazo zimejikita katkka kutoa elimu Ya ubunifu huku zikilenga kuhimiza na kuchochea ari ya nidhamu, umakini , ufanisi , uwezo , juhudi, weledi , uwajibikaji n.k

“Hii itafungua njia katika safari ya kufikia maendeleo endelevu na kuifanya Tanzania kuwa mshindani katika ngazi za kikanda na kimataifa ikidhihirisha kma mshiriki hai katika nyakati hizi za utandawazi “ Amesema

Kongamano hilo limeenda sambamba na kaulimbiu isemayo “kuza na fanya ubunifu: Uhandisi bora katika Dunia inayobadilika , ambapo kutokana na kaulimbiu hiyo, Moses lisema “Tunapaswa kufahamu kuwa utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya maendeleo unahitaji siyo tu kukuza ujuzi na maarifa katika uhandisi bali pia kuluza kiwango na uwezo wa ubunifu wa kisayasi na teknolojia na ujuzi nyingine muhumu za Karne ya 21 “

Kadhalika, Mozes aliwataka wahandisi na wadau wote wa sekta mbalimbali za uchumi nchini kwenda kushiriki kwenye komgamano hilo huku akiwakumbusha wahandisi na mafundi ambao hawajajiunga na taasi ya (IET)wajiunge na taasisi hiyo.
Previous Post Next Post