Na Lilian Ekonga, Dar es salaam.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwingulu Nchemba anatarijiwa kutunuku vyeti kwa wahitimu 417 katika mahafali ya 17 ya chuo cha Kodi (ITA) katika ngazi ya stashahada, shahada na stashahada ya uzamili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo novemba 20 Jijini Dar es salaam, Mkuu wa chuo kodi Isaya Jairo, amesema mahafali hayo yatafanyika Novemba 22, 2024 ambapo wahitimu watakao tunukiwa wanaume wakiwa 236 na wanawake 181.
"Mheshimiwa Waziri pia atato zawadi kwa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea na masomo waliofanya vizuri zaidi katika mwaka wa masomo 2023/2024 pamoja na wahadhiri wa chuo waliotoa machapisho mbalimbali"amesema Jairo.
Ameongeza kuwa wahitimu 195 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki, wahatimu 28 watatunukiwa cheti cha usimamizi wa forodha na kodi, wahitimu 61 watatunukiwa stashahada ya usimamizi wa forodha na kodi na wahitimu 119 wakitunukiwa shahada ya usimamizi aa forodha na kodi.
Amesema Chuo cha Kodi kinajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tano wa Chuo ambao umejikita katika kutoa matunzo kwa njia ya kisasa za kidijitali.
"Tunatarajia mafunzo ya elimu masafa (onlineDistance Electronic Learning) yatakapoanza yataongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mafunzo katika chuo pamoja na kufikia wanafunzi wengi kwa njia rahisi, kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu na hivyo kuongeza idadi ya wahitimu" amesema
Jairo amesema kuanzishwa kwa mafunzo hayo kielectroniki ya masafa huria mwaka huu utasaidia kuongeza uandikishaji wa wanafunzi kwa mwaka kutoka 5000 hadi 7000 na kupanua ufikiaji wa programu maalim za mafunzo ya ITA.
Aidha ameibanisha ushirikiano wa ITA na somaliland katika kutengeneza mfumo thabiti wa usimamizi forodha na kodi.
Amebainisha kuwa kufanya kazi na nchi kama Somaliland, Zanzibar,Bostwana na malawi, ITA Inaendelea kuchukua jukumu muhimu katika kuboresha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha mifomo ya kodi barani Afrika.