Na Lilian Ekonga, Dar es salaam
Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Shemata Khamisu amesema Serikali ya Zanzibar imetekeleza afua mbalimbali katika kuhakikisha tasnia ya kuku inakua na kuleta tija kwa kuwajengea uwezo wa wataalamu wa mifugo wa ndani katika mbinu za kisasa za ufugaji bora na udhibiti wa magonjwa.
Alikadhalika kuweka mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa ya kuku na ndege wafugwao ili kudhibiti milipuko ya magonjwa pamoja na kuimarisha utekelezaji wa afua za Afya.
Waziri ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2024 jijini Dar es salaam, wakati akihitimisha Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na Nsege wafugwap kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeweka mikakati mbalimbali katika kuhakikisha Tasnia hii ya kuku na ndege wafugwao inakua na kuchangia zaidi katika ajira, uchumi na kuimarisha usalama wa chakula na lishe.
"Mkakati hiyo ni Kuanzisha mashamba ya kuku, Uwekezaji katika maeneo ya kutotoleshea vifaranga vya kuku,Kuanzishwa kwa kiwanda kipya cha vyakula vya mifugo,Kuanzishwa kwa machinjio mapya ya kuku, Kuwekeza katika maabara ya mifugo na uwezo wa uchunguzi, pamoja na uzalishaji wa chanjo za mifugo pamoja na Kuanzisha vituo vya utafiti wa kuku.
Aidha amesema kuna Mikakati ambayo serikali ya zanzibar inatekeleza pamoja na Kufungamanisha kanuni na viwango vya ufugaji kuku katika nchi za SADC ili kuwezesha biashara za kikanda na kuhakikisha usalama wa mazao ya kuku na bidhaa zake.
"Kuanzisha programu za pamoja za utafiti kati ya nchi za SADC ili kushughulikia changamoto zinazofanana zikiwemo udhibiti wa magonjwa, mbinu na teknolojia za kuboresha ufugaji.
Kuendeleza programu za mafunzo za kikanda kwa wafugaji, madaktari wa mifugo, na wafanyakazi wa ugani ili kuongeza ujuzi katika usimamizi wa kisasa wa kuku na ustawi wa wanyama" ameongeza
Pia ametoa rai kwa Jumuiya za Kikanda na Kimataifa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha tasnia ya kuku na ndege wafugwao, ili kupunguza ma kuondoa changamoto, vikwazo vilivyopo katika tasnia ya kuku.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa AGRA Tanzania Bw. Vianey Rweyendela amesema