NAIBU KATIBU MKUU UCHUKUZI ATEMBELEA OFISI ZA TMA



Dar es Salaam, tarehe 30 Oktoba 2024.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Ndg. Ludovick Nduhiye amefanya ziara ya kutembelea ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zilizopo katika jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam ikiwa ni moja ya malengo yake ya kuzitambua Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Uchukuzi, kufahamu majukumu ya kiutendaji na kuelewa changamoto zinazowakabili na Mikakati ya kuimarisha Taasisi na utoaji wa huduma.

Baada ya taarifa ya utendaji kutoka TMA, Naibu Katibu Mkuu, Uchukuzi aliipongeza TMA kwa kuendelea kuimarisha na kuboresha huduma za haki ya hewa nchini, ikiwemo kuongeza usahihi wa utabiri,  akieleza kuwa yeye ni mmoja wa wadau wa Mamlaka na anafuatilia, kuzingatia na kutumia taarifa za hali ya hewa.

'Kiuekweli taarifa zenu ni nzuri, niwapongeze sana TMA, mimi ni mdau wa taarifa zenu na nimekuwa nikizifuatilia, kuzizingatia na pia kuzitumia, naweza kusema TMA ya sasa si kama ile za zamani." Alisisitiza Ndg. Nduhiye.

Aidha, akiwasilisha awali salamu za ukaribisho Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a alieleza  Maono na Mikakati ya kuimarisha huduma na kuongeza ushawishi wa TMA na Tanzania katika masuala ya hali ya hewa kikanda na kimataifa. Aidha alisisitiza azma ya kuifanya Tanzania kuwa HUB ya mafunzo ya Rada za hali ya hewa katika Afrika. 

Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Ofisi za Zanzibar Ndg. Masoud Faki alihitimisha kwa kutoa salamu za shukrani kwa ndg. Nduhiye,  kwa kuitembelea TMA ndani ya muda mfupi tokea ateuliwe kama Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yake.
Previous Post Next Post