RAIS SAMIA: KILA ALIYEPASWA KULIPWA FIDIA ATAPATA FAIDA YAKE


“Niwashukuru wananchi kwa kupisha miradi iendelee kwa kusubiri fidia zao. Nataka niwahakikishie kwa kila anayepaswa kulipwa fidia atapata fidia yake, hakuna mradi utakaopita serikali ikachukua ardhi bila kulipa fidia.

“Tunaweza tukachelewa kulipa, kwasababu fedha zinakwenda kwenye mradi kwanza, lakini tutalipa fidia zote. Ombi langu kwenu ndugu zangu tufanye kazi, tuzalishe, tulime mazao mengi, tuuze kwa wingi, tufanye kazi tuuze nje tupate fedha nyingi ili tuweze kufanya mambo yetu ya ndani.

“Kwasababu miradi mingi tunayofanya ni ya fedha za kukopa nje, kwahiyo tunashindwa kwa mapato ya ndani jinsi ya kulipa fidia, lakini kwa jinsi tunavyokusanya ndivyo tunavyolipa fidia

“Kwahiyo tukizalisha kwa wingi, tukifanya kazi kwa wingi, fedha ikipatikana kwa wingi fidia hizi zitalipwa kwa mara moja. Lakini niwahakikishie kila mwenye haki yake atakwenda kupata haki yake,” amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiweka jiwe la Msingi katika mradi wa maji wa Mtyangimbole Songea mkoani Ruvuma
Previous Post Next Post