KONGAMANO LA PILI LA UTENGAMANO( REHABILITATION SUMMIT) KUFANYIKA SEPTEMBA 18


Na lilian Ekonga

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Rihab Health imeandaa Kongamano la pili la Utengamao (Rehabilitation  summit) lenye lengo la kuwakutanisha  wataalam, watoa huduma za afya, watunga sera, na washirika mbalimbali ili kujadili mikakati ya kuendeleza huduma za utengamao chini Tanzania.

Akizugumza na Waandishi wa Habari leo  septemba 11 jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Rihab Health amesema kongamano linalenga kuimarisha mfumo wa afya kwa kuhakikisha huduma za utengamano zinafika ngazi za msingi za huduma za afya  ya akili

"Kongamano la pili la utengamao yaani "Rehabilitation Summit" litafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Septemba 2024 katika ukumbi wa JNICC lenye kauli ya 'Kuendeleza ajenda ya utengamao, kuimarisha mifumo ya Afya nchini." amesema  Remla

Ameongeza kuwa Katika kongamano hilil kutakuwa na  mijadala mbalimbali itakayojadili masuala ya  Jinsi ya kuongeza upatikanaji wa huduma za utengamao katika maeneo ya vijijini na yenye uhaba wa rasilimali, Kuimarisha shirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ili kuboresha miundombinu ya huduma za utengamao, Kutoa mapendekezo muhimu ya kisera na hatua za kuboresha huduma za utengamao chiniTanzania, Nafasi ya teknolojia na uvumbuzi katika kuboresha huduma za utengamao.

Kwa upande Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt Nyembea amesema wizara ya afya inatambua na kuthamini mchango wa huduma za tengamao katika kuimarisha mfumo wa afya.

"Huduma hizi ni muhimu kwa kuweza kutibu na kusaidia watu wenye maradhi ya mda mrefu, mjeraha ya mda mrefu na kuweza kuwarejeshea hali zao za kawaida na kuboresha maisha yao."amesema Nyembea

Ameongeza kuwa serikali  kupitia wizara ya afya imekuwa ikiweka msisituzo mkubwa katika kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora hasa huduma za utengamao ili kuweza kukidhi mahitaji ya watanzania wote pasipo kubagua.

"Kwenye kongamano hilo litazinduliwa na Waziri wa Afya  siku ya tarehe 18 na ndiye atakuwa mgeni rasmi wa Kongamano hili ambalo ni muhimu katika kubirosha mfumo wa afya nchini." amesema

Nae  Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Kikosicha Usalama Barabarani Tanzania , Deus sokoni amesema katika kuhakikisha afya ya mtu inatengamaa  jeshi la Polisi linahusika katika kulinda maisha ya mtu na mali zake kwa wanavyo tumia barabara kwa maana ya kikosi cha usalama barabarani.

"Katika matumizi ya barabara tumekuwa kukishuhudia changamoto mbalimbali ambazo zingine niwachia ulemavu wa kudumu kwa watu na wajibu wetu ili kupunguza changamoto hizi ni kupata elimu ya usalama barabarani kwa watu, waendesha magari na watembea  kwa miguu."amesema

Aidha amesema takwimu ziwe zinaenda na takwimu zingine za usalama barabara katika kuhakikisha tunaboresha huduma za kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara.
Previous Post Next Post