ZAID YA WATU 1000 KUKIMBIA MBIO ZA USIKU "DAR NIGHT RUN" AGOSTI 31


Na Lilian Ekonga, Dar

Uongozi wa The  Runners Club  waandaji wa mbio mbalimbali wametangaza  Mbio za  Usiku  "DAR NIGHT RUN" kwa awamu ya 7  zenye lengo  la kujenga ya afya mwili na kuburudisha watu wanaofanya mazoezi

Akizunguza na waandishi waandishi Msemaji wa The Club Runners Godfrey  Mwangungulu , amesema mbio hizo  zinatarajiwa kukusanya watu 1200 na  zitafanyika  tarehe 31 Agost kuanzia saa nne mpaka saa sita usiku  katika viwanja vya Police mess jijin Dar es salaam.

"Hii ni moja ya sikukuu kubwa sana  ya mbio ya  kipekee  ambayo inafanyika usiku na hakuna mbio nyingine ambayo inafanyika usiku kwa hapa Tanzania, na limekuwa tukio kubwa sana linalovutia watu wengi hapa Tanzania" amesema.

Ameongea  kuwa mbio zitanzia kilometa 10 mpaka kilometa 15 ambapo kwa  mtu ambaye anataka7 kujisajili kwenye mbio hizo  anaweza kufuatilia mtindao yao ya kijamii ya Tha Runners Clun kwa kupata taarifa zaid n kuweza kujisajili kupitia website yao kwa shilingi 45000.

Aidha amesiitiza kuwa kutakuwa na usalma wa kutosha kwenye mbio hizo za kwakuwa zinafanyika katika eneo la polisi na usalama utakuwepo wa kutosha kwenye sehem mbazo watu watakuwa wanakimbia.
Previous Post Next Post