DOTTO MAGARI AWATAKA CHADEMA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA 'MAZINGIRA BORA YA UWEKEZAJI'


Na Mwandishi Wetu,

Mfanyabiashara  maarufu wa Magari Tanzania Dotto Keto maarifu kama Dotto Magari, amewataka Chama cha demeokrasia  na Maendeleo CHADEMA kumuunga Mkono Rais samia suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutiwa wawekezaji kuja kufanya biashara nchini.

Aidha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan msa kuhakikisha nchi i akuwa ma amani hivyo amewataka chama CHADEMA  Kuacha  siasa za uongo  na kumpa Rais Samia kongole kwa kazi kubwa anayifanya.

Magari amesema ;” Nyinyi majirani zetu mlikua hamna ofisi
Kwa takribani miaka 30, leo mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa mikocheni mnataka nini majirani? 

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia,  hiyo siyo amani? .

Ameongeza kuwa  Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi.

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” Amesisitiza
Previous Post Next Post