Na Humphrey Msechu, Dodoma
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Yusuph Mwenda, awaasa wakulima kutembelea banda lao kwa lengo la kupata elimu lilopo kwenye viwanja vya nzuguni jijini Dodoma
Amesema hayo Leo alipotembelea Banda la TRA lililopo kwenye viwanja vya nanenane jijini Dodoma na kuwaasa wananchi waje wapate elimu ya kawaida ya kodi na elimu ya mabadiliko ya sheria iliyofanywa na bunge la Jamhuri ya Tanzania lakini wataipata hapa.
Pia watapata huduma ya kukadiliwa kiasi ambacho wanapaswa kulipa ikiwemo kupatiwa Tini na huduma zingine za kielimu ambazo zitawafanya wawe na uelewa ili waweze kuchangia kulipa kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi yao.
Sambamba na hilo amempongeza Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo kukutumia kodi na kufanya maendeleo makubwa kama miundombinu ya barabara, elimu kwa ajili ya watoto, sekta ya afya na yote hayo ni uthibitisho wa yale anayoyafanya.
Ameongeza kuwa maendeleo yote yanayopatikana yasingeoneka pasipo ukusanyaji wa kodi lakini sio tu kukusanya kodi bali matumizi mazuri ya kodi
Ametoa wito kwa watanzania kudai risiti pindi wanapo fanya manunuzi kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamechangia kwa lengo maendeleo ya nchi yao.