FCC YAZIDI KUTUO ELIMU YA BIDHAA BANDIA KWA WAKULIMA, WAVUVI NA WAFUGAJI


Na Humphrey Msechu, Dodoma

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Ushindani( FCC), William Erio, ametoa elimu ya namna ya kuepukana na bidhaa bandia kwa wakulima, wafugaji na wavuvi jijini Dodoma.

Erio ametoa elimu hiyo katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yajulikanayo kama nane nane yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni Dodoma.

Amesema katika kuepuka bidhaa bandia wadau mbalimbali wanapaswa kununua bidhaa zao kutoka kwa wazalishaji wenyewe au wale walioidhinishwa na wazalishaji ili wapate vitu vitakavyowasaidia kuwa na bidhaa bora.
"Kama tume tumeshiriki katika maonesho haya kwa kutoa elimu kwa umma kuelimisha kuhusu shughuli za taasisi kuwa ni pamoja na kulinda na kushajihisha ushindani, kwa sababu watu wanatengeneza biashara zinazofanana

"Vile vile tumetoa elimu jinsi ya kumlinda mlaji. Kubwa tumewaambia wao kuhusu kuepukana na bidhaa bandia, kwa sababu wapo katika uzalishaji wanaweza wakaagiza bidhaa wanazitumia.

"Katika uzalishaji bidhaa hizo kama zitakuwa bandia, zitafanya bidhaa zao zikose ubora," amesema.

Amesema kwenye kilimo wakulima wakipata pembejeo sahihi watazalisha vizuri, zikiwa bandia au za kughushi watakosa mapato mazuri.
"Tumewaeleza kuhusu vifungashio kwamba wahakikishe vinakidhi viwango wala hakuna anayeweza kughushi ili kuwaharibia soko," amesema.
Previous Post Next Post