DKT. JIM YONAZI AWAKUMBUSHA VIONGOZI OFISI YA WAZIRI MKUU KUWA VIONGOZI BORA ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt Jim Yonazi akihitimisha kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya hiyo, watumishi na Taasisi zilizo chini yake, Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.

Baadhi ya Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakiwa katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya hiyo, watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika  Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge an Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa akitoa neno la shukrani katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya hiyo, watumishi na Taasisi zilizo chini yake, Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.


Muwezeshaji wa mada inayohusu staili ya maisha na Nidhamu ya vyakula Dkt Dk. Fredrik Lazaro Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili akitoa mada katika  kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.

Sehemu ya Washiriki katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akigawa vyeti kwa viongozi wakati wa kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Na; Mwandishi Wetu – Arusha


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi  amewataka viongozi wa Ofisi hiyo kufanya kazi katika ubora na ueledi wa hali ya juu ili kufikia malengo ya Serikali katika kuwahudumia Watanzania.


Ameyasema hayo mapema leo tarehe 1 Agosti 2024 Jijini Arusha alipohitimisha kikao za mazingativu (Retreat) kilichohusisha viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Menejimenti, Watumishi na Taasisi zilicho chini ya Ofisi hiyo.


Dkt. Yonazi alisema kuwa ana imani kubwa kwa watumishi na viongozi wa Ofisi hiyo kuwa watakuwa ni watumishi wenye thamani na utulivu na wenye nia ya kuwatumikia Watanzania kwa weledi na moyo Thabiti. 

“Sisi hapa wengi ni viongozi, watu wa chini yetu ndo wametuwezesha kuwa viongozi hivyo tumesiweke mazingira magumu kwa waliyopo chini yetu katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.” Alibainisha Dkt. Yonazi


Aidha, Dkt. Yonazi aliwashukuru Viongozi wa juu wa Ofisi hiyo kwa Maandaliz mazuri ya kikao hicho cha siku tatu cha mazingativu kilichokuwa na lengo la kuendeleza mafunzo kazini kuwaleta watumishi na viongozi pamoja kwa ajili ya kujifunza na kuwa na mbinu ambazo zitaweza  kuboresha utendaji wa shughuli za kila siku za Ofisi.


Awali akizunguza katika kikao kazi hicho  Mkurugenzi wa Mipango na Bajeti kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Eleuter Kihwele amesema mafunzo hayo yalishafanyika mwaka 2023 na yamesaidia sana katika kuboresha utendaji kazi na kusaidia kuimarisha umoja kwa kuwaleta pamoja watumishi wote.

Aliongezea kuwa utendaji wa pamoja katika maana ya viongozi na watumishi kukaa pamoja kujadili pamoja namna ya kuleta Tija katika uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa shughuli za Serikali unachochea ufanisi kazini na kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.
Previous Post Next Post