Naibu Waziri Ummy Akagua Maandalizi Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa 2024


Na Mwandishi wetu-OWM

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga leo tarehe 10 Julai, 2024 amekagua maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa inayotarajiwa kufanyika tarehe 25 Julai, 2024 jijini Dodoma.

Mhe. Ummy ameridhishwa  na maandalizi hayo yanayoendelea na anaimani kwamba maandalizi hayo yatazidi kufanyika vizuri na yatakamilikalika kwa wakati.


Aidha, maadhimisho hayo yatashirikisha gwaride la Majeshi ya Ulinzi na Usalama lenye vikosi vitano ambavyo ni  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Poliosi, Jeshi la Magereza pamoja na jeshi la Uhamiaji.
Awali akitoa  maelezo kuhusu maandalizi hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Batholomeo Jungu amebainisha kuwa, maadhimisho hayo yatatanguliwa na uwashaji wa Mwenge siku ya tarehe 24 Julai, 2024 usiku ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatafanyika tarehe 25 Julai, 2024 jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan.

Previous Post Next Post