KAMPUNU YA SANLAM IMEZINDUA MFUKO UTAKAO WASAIDIA WATANZANIA KUJIKWAMUA KIUCHUMI


Na Lilian Ekonga- Dar es salaam.
 
Kampuni ya Sanlam Tanzania imeiahidi Serikali kushirikina nayo ili kuweka Mazingira wezeshi yatakayoweza kuwasaidia Wananchi  kujikwamua Kiuchumi.

Ameyabainisha hayo Afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya masoko ya mitaji  na dhamana Tanzania Nicodemus Mkama Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Mfuko wa Sanlam Investment ambapo amesema utawezesha kutoa fursa kwa Vijana na Wanawake kwenye kuwawezesha Kiuchumi kwa kuwapa gawio.

Mkama amesema Mfuko huo utaiwezesha Serikali kupata fedha pindi Wananchi watakapo jitokeza kuwekeza na fedha ambazo  zitasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo hapa Nchini.

"Tutahakikisha Kampuni yetu ya Sanlam inashirikiana vizuri na Serikali na kuleta Maendeleo kwani Mfuko huu umekidhi vigezo katika kukuza bidhaa zake Kwa Umma," amesema Mkama.

Nae Mwenyekiti wa Sanlam East Afrika  Julius Magabe amesema Sera yao inahakikisha huduma zao zinatolewa katika Taasisi, Makampuni, Watu binafsi na Vikundi ambapo lengo ni kuleta Mapinduzi katika Uwekezaji hapa Nchini 

"Huduma hizi tunazileta zitasaidia Jamii na kuwezesha Wananchi kupata Gawio ambapo Soko la Tanzania linatoa fursa wezeshi za Kiuchumi hivyo tumefungua milango ya kuwafikia Watanzania kuanza kuwekeza Kwa kiwango cha chini kuanzia shilingi elfu kumi ya Kitanzania," amesema Magabe.

Ikumbukwe kuwa Kampuni ya Sanlam Tanzania Kwa kushirikina na Benki ya CRDB imezundua Mfuko wa Sanlam Investment kwa lengo la kuwasaidia Watanzania kuweka Mitaji ili baadae waweze kupata faida ya gawio kulingana na Mitaji yao.
Previous Post Next Post