BENKI YA TCB YAZINDUA HUDUMA YA TCB POPOTE, KUMUWEZESHA MTEJA KUJIFUNGULIA AKAUNTI


Na Mwandishi wetu, 

Takwimu zinaonyesha kuw Asilimia 89 ya watanzania wanapata huduma za kifedha ndani ya kilometa tano huku asilimia 22 ya watanzania wana akaunti za kibenki .

Ameyasema hayo  leo Julai 30,2024 Jijini Dar es  salaam , Jesse Jackson Afisa Mkuu wa huduma za kidigitali na ubunifu kutoka Benki ya Biashara ya Taifa (TCB) wakati wakizindua  huduma ya TCB popote akaunti itakayo muwezesha mtumiaji kupata huduma za kifedha kupitia simu janja  mkononi.

"Akaunti ya TCB Popote inamwezesha mtu yeyote aliye na simu janja kufungua akaunti mahala popote na wakati wowote bila haja ya kwenda katika tawi la benki. Huduma hii itawasaidia hasa wale waishio vijijini na walio mbali na benki kupata huduma za kibenki bila shida yoyote." amesema jackson.

Ameongeza  kuwa bado nchini kuna uhitaji huduma za kifedha ndio maana wamezindua huduma hiyo itakayomwezesha na kumrahisishia mtanzania kufanya huduma popote na kwa urahisi pamoja na masuhishi ya kifedha.

Jacksoni amesema Wateja wanaweza kuanza kutumia akaunti zao walizofungua mara tu baada ya kukamilisha zoezi hilo kwa kuweka TZS 1,000 kama salio la kuanzia. 


Aidha amesema huduma hiyo itamwezesha mteja wao kulipia tiketi za kieletroniki za treni ya umeme SGR hivyo kumrahisishia mda wa kwenda kukata tiketi

Kwa upande wake  Deo Kwiyukwa Mkurugenzi wa masoko na ukuzaji wa biashara na masoko kutoka TCB amesema  huduma hiyo ya TCB popote itawasaidia watanzania wengi kurahisisha kupata huduma kwa uharaka na na unafuu na Benki hiyo imefanya hivyo kuweza  kurahisisha upatikani wa huduma zao na kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Previous Post Next Post