BENKI YA MAENDELEO YAWEKA HISTORIA KWA KUPATA FAIDA YA BILIONI 2.35


Na Lilian Ekonga,Dar es salaam.

Benki ya maendeleo imeweka historia ya kuwa benki yenye faida kwa miaka 9 mfululizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 ambapo kwa mwaka 2023 imepata faida ya shilingi Bilioni 2.35 na gawio lake kwa asilimia 50 ikiwa ni shilingi Bilioni 1.17 sawa na shilingi 44 kwa kila hisa.

Aidha mwaka jana Benki hiyo ilitoa shilingi 26 kwa kila hisa moja sawa na ongezeko la asilimia 69.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Peter Tarimo wakati akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaama kuhusu  gawio kwa wanahisa kwa mwaka 2024 kutokana na faida ya mwaka 2023.

Tarimo aliainisha baadhi ya vichocheo vya mafanikio hayo makubwa ambayo ni pmaoja na Ukuaji wa faida baada ya kodi kwa asilimia 66 kutoka Shilingi za Kitanzania bilioni 1.4 mwaka 2022 hadi Shilingi bilioni 2.3 kwa mwaka 2023.

Ameongeza kuwa  kuongezeka  kwa Amana za Wateja kwa asilimia 15 kutoka Shilingi za Kitanzania bilioni 78.0 mwaka 2022 hadi Shilingi za Kitanzania bilioni 90.0 mwaka 2023.

Pia amesema  vichocheo vingine ni  “Kumarika kwa ubora wa mikopo kutoka mikopo chechefu ya asilimia 5.2 mwaka wa 2022 hadi asilimia 4.95 mwaka wa 2023 - hii imechangiwa na kuimarika kwa hali ya uchumi na kuwafanya wateja walipe mikopo kwa wakati, Kuongezeka kwa mikopo kwa wateja kwa asilimia 21 kutoka shilingi za kitanzania bilioni
61.0 hadi shilingi za kitanzania bilioni 74.0 mwaka 2023.”

“Kuongezeka kwa jumla ya mali za benki kwa asilimia 17 kutoka Shilingi za Kitanzania bilioni 107.0 mwaka 2022 hadi Shilingi bilioni 125.0 mwaka 2023 na Kuimarika kwa mtaji wa benki kwa asilimia 12 kutoka Shilingi za Kitanzania bilioni 17.0 mwaka 2022 hadi Shilingi bilioni 19.0 mwaka 2023.”

Aidha amesema Benki imeendelea kuwekeza kwenye teknolojia ambapo sasa wako kwenye hatua za mwisho katkka kuanzisha huduma mpya za kidijitali kama Benki ya mtandao (internet Banking), mfumo wa ukusanyaji wa malipo ikiwemo ada za shule na mikopo kwa njia ya simu 

“Hii itawezesha benki kuongeza faida kwa fedha za wanahisa kwa mwaka 2024 na kuboresha njia mbadala za upatikanaji wa huduma kwa wateja wetu”

Kadhalika, Katika juhudia za kuboresha huduma, Tarimo amesema kwa sasa wmefungua tawi jipya Mbagala ambalo tawi hilo ni
La tano wakiwa na lengo la kuwasogezea huduma wateja wake, wakazi wa mbagala na maeneo jirani lakini pia wanampango wa kufungua matawi mengine nje ya Dar es Salaam.

Kwa upande wake Meneja Usajili wa Hisa na Hati fungani kutoka CSDR, Gideon Gapange amesema  hisa hizo zinaanza kuuzwa kwa siku 14 ambapo mtu akishanunua hisa za maendeleo bank katika kipindi hiki atastahili kulipwa lile gawio linalotewa kutokana na mahesabu ya mwaka yaliyoishia Desemba mwaka 2023.

Pia amesema kuanzia tarehe 14 Agost hisa zitaanza kuuzwa bila gawio mpaka katika kipindi kinachoendelea huku daftari la wanahisa likifungwa tarehe 6 Agost.

Aliongeza kuwa Wanahisa wote wanaostahili kupata gawio wale ambao hawajaboresha kumbukumbu zao kwenye daftari la wanahisa wanatakiwa kuboresha kumbukumbu zao kwa kuwapatia namba zao za simu, bank account ili waweze kupata gawio kwa urahisi zaidi
Previous Post Next Post