WANAWAKE WAJASIRIMALI 675 WAWEZESHWA MASHINE NA VYEREHANI KUTOKA CHINA.


Na Lilian Ekonga, Dar Es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amepokea msaada wa Vyerehani 425 na mashine za kutotolesha vifaranga 250 kwa ajili ya wanawake wajasiriamali nchini.

Msaada huo uliotolewa na Serikali ya China, wenye thamani ya Tsh. Mil. 79 umekabidhiwa na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Chen Mingian katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Dar es Salaam Aprili 29, 2024.


Akipokea msaada huo, Waziri Dkt. Gwajima amesema Tanzania inatambua umuhimu wa Wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi hivyo msaada huo utakuwa chachu kwenye program ya uwezeshaji wanawake kiuchumi inayoongozwa na na Kinara wa Dunia na Taifa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ambapo, itawaongezea ari wanawake kwenye kuongeza uzalishaji na ushonaji wa nguo na uzalishaji wa vifaranga hivyo kuongeza pato na kuchangia uchumi wa Taifa.


“Tukio hili ni muendelezo wa mahusiano mema ya muda mrefu kati ya Tanzania na China. Msaada huu ni chachu kwa wanawake wa Tanzania kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati vya ushonaji na udarizi nguo" amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Previous Post Next Post