UCHAGUZI WA BARAZA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUANZA Me 21 2024


BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali linatarajia kufanya uchaguzi wake wa kupata viongozi wapya kwenye ngazi za wilaya, mkoa na taifa kuanzia Mei 21 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa kamati ya mpito ya kuratibu Uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali,Christina Kamili Ruhinda,amesema uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa kanuni ya 5(a)(iv),5(b)(ii) na 5(c) (v) ya kanuni za uchaguzi za mwaka Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2016,Baraza linatakiwa kufanya Uchaguzi kila baada ya miaka mitatu huku uchaguzi awali ulifanyika june 2021.

Ambapo amesema tarehe 7 mei 2024, baraza ilifanya uteuzi wa kamati ya mpito ya kufanya uchaguzi inaudwa na wajumbe kumi ambao ni viongozi wa mashirika yasiyi ya kiserikali ya kitaifa na kimataifa huku ikitakiwa kukamilisha mchakato wa uchaguzi kabla ya tarehe 30 june 2024.

Ruhinda,amesema kamati yake inawataka mashirika yasiyo ya Kiserikali na umma kwa ujumla kuhusu kuanza mchakatato wa Baraza hilo kufuata ratiba na mambo muhimu kuhusu Uchaguzi huo kupitia kwenye tovuti.
" Vigezo na sifa za wagombe ambapo atakiwa awe kiongozi au mwanachama wa shirika lisilo la kiserikali liliojaliwa chini ya sheria ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Awe umri usiopungua miaka 18 uziozid miaka 70, asiwe amepatika na kosa la jinai, awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea, awe na uwezo mzuri wa kuzungumza lugha ya kiswahili na kingereza na awe na akili timamu"amesema Ruhinda


Aidha amesema Fomu za maombi zitalowa bure na msimamizi wa uchaguz, zoezi la kuchukua fomu litaaanza saa 2 hasubuhi kumaliza saa 9 kamili huku fomu ya ngazi ya taifa itapatikana kwenye tovuti ya baraza www.makongo.or.tz, na kurudishwa kwenye email uchauzi makongo@gmail.com.

"Kamati pia inatoa wito kwa Viongozi na Wanachama wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi wa Baraza kuanzia ngazi za Wilaya,Makundi maalum,mkoa hadi Taifa
Previous Post Next Post