TMA YATOA TAHADHARI YA UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"


Na Mwandishi Wetu, Dar

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imesema hali ya Kimbunga iliyotabiriwa jana Mei Mosi 2024 inaendelea kuimarika na kwamba Kimbunga hicho sasa kinaikaribia Pwani ya Mkoa wa Mtwara.

Taarifa ya mwelekeo wa Kimbunga hicho kinachoendelea kuimarika na kuwa cha kiwango cha kati kwa sasa kipo umbali wa Kilometa 506 Pwani ya nchi ya Tanzania.

Kutokana na hilo TMA imetoa tahadhari kwa taasisi zinazojihusisha na masuala ya majanga kuendelea kufuatilia taarifa za Kimbunga hicho huku ikiwataka watu wanaofanya shughuli za usafirishaji baharini na wavuvi na wanaoishi maeneo ya Pwani ya bahari ya Hindi kuendelea kuchukua tahadhari wakati Kimbunga hicho kikitarajiwa kuingia usiku wa leo Mei 03.



Previous Post Next Post