BENKI YA TCB YAZINDUA KAMPENI YA KABAMBE YA KIKOBA KIDIGITAL


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Katika kuendelea kuboresha huduma za kigitali,Tanzania commericial Bank[TCB] imezindua kampeni ya TOBOA NA KIKOBA, yenye lengo la kutoa huduma ya kikoba kidigitali ambapo vikundi vinaweza kuweka akiba kwa Pamoja kwa kupitia mitandao  ya simu Tigo,Airtel, Halotel Pamoja na  Vodacom,

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mey 9 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TCB Adam Mihayo amesema lengo la kampeni ni kuwazesha watanzania kufanya miamala yao ya vikundi, kuweka akiba na kuweza kukopeshana katika vikundi vyao.

“Tuliona watanzania wengi kutokana na Maisha yao wanapenda kuwa na vikundi mbalimbali tukaona tuje na kampeni hii ili waweze kufanya miamala hii kidigitali ili waweze kufanya miamala kwa haraka na uwazi ili kila mtu kwenye aweze kufahamu kuhusu miamala hiyo” amesema Adam Mihayo.

Ameongeza kuwa dhumuni kubwa  la kampeni hiyo ni kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa kushirikiana na kampuni za simu ili kuhakikisha wananchi  wanapata  hiuduma bora ya kikoba digitali.


Ameongeza kuwa dhumuni kubwa la kampeni hiyo ni kuongeza ujumuishaji  wa kifedha kwa kushirikiana na kampuni za simu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya kikoba kidigitali.

Aidha amesema huduma itakuwa salama kwa kufuata misingi na taratibu zote za kibenkiwateja wote watakao jiunga kupitia hivyo vikundi fedha zao zitakuwa salama

"Tutafika nchi nzima ili watanzania waweze  kuelewa kampeni hii ya Toboa kikoba ni nini na namna ya kujiunga na vikundi,tumekuja na utaratibu mzuri kila mtu aliyepo kwenye mtandao wowote aweze kujiunga.

Kwa upende wake katibu wa Good hope vikoba Tabata Sonia Choteka amesema Benki ya tcb imewasaidia sana kwa  kuletea huduma hii ya vikoba kidigitali kwa sababu itawasadia  kuwakutanisha wote kwa pamoja hata wakiwa na mitandao ya simu tofauti.
Previous Post Next Post