HAKI ELIMU: MABORESHO KATIKA BAJETI YA SEKTA YA ELIMU MWAKA WA FEDHA 2O24/25


Na Lilian Ekonga

Katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 serikali imeshauriwa kutenga Bajeti  kwa ajili ya kutoa mafunzo kazini kwa walimu waliopo ili waweze kusaidia utekelezaji wa tahasusi na kuajiri walimu wapya wenye ujuzi umahairi katika tahasusi husika. 

Hayo ameyasema , Mkurugenz Mtendaji  wa Hakieleimu Dkt John Kalage, wakati akitoa  mapendekezo  juu ya  upangaji  na utendaji  bajeti  ya sekta  ya Elimu  ya Mwaka  wa Fedha 2024/25 leo aprili 23, 2024 jijin Dar es salaam.

"Ikumbukwe kuwa Hadi Februari, 2023 mahitaji ya walimu katika shule  za sekondari yalikuwa ni 174,632 ambapo walimu waliopo ni 84,700 na upungufu wa walimu 89,932 sawa na asilimka 51.5%" amesema  Dkt Kalege. 

Pia Haki Elimu wameshauri   uwepo mpango maalumu wa kuhamasisha  udahili wa wanafunzi wa ualimi vyuoni ili kuendelea kutengenezq walimu wenye ujuzi mahususi kulinganq na mabadiliko ya tahasusi. 

Aidha wameiomba  serikali kutenga bajeti  maalum kwajili ya uchapaji nq usambazaji  wa vitabu vya kiada mashuleni kwa kuzingatia vitabu hivyo ni vipya na havina akiba ya vitabu mbadala. 

"Kuweka Mpango maalumu wa usambazaji wa vitabu hivi mashuleni ukianisha muda mahususi wa ukamilishaji wa zoezi hili" amesema. 

Mbali na hayo, Hakielimu wamependekeza ujumuishi wa teknolojia katika utekelezaji wa mtaala mpya wa Elimu, ambapo imeishauri serikali kupitia Wizara za Sekta ya elimu kutenga Bajeti kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi na sekondari ili kuziandaa na utoaji wa Elimu kwa Mtaala mpya na matumizi ya teknolojia.

Vilevile HakiElimu imependekeza Serikali itenge Bajeti kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia vya teknolojia lakini pia kuanzisha vipindi vya ujuzi wa matumizi ya mtandao ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na umahiri wa kutumia mtandao kwa usahihi, uwezo wa kutatua matatizo na uwezo wa kujifunzia.
Previous Post Next Post