MKURUGENZI MKUU NHC ZIARANI MIKOANI KUKAGUA UTENDAJI KAZI



Na Mwandishi Wetu, Moro

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHC) Bw. Hamad Abdallah leo ameanza ziara ya kikazi mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida akiwa mkoani Morogoro amefanya ziara Ofisi za NHC Morogoro kujua utekelezaji wa mipango ya Shirika na namna ya kutatua changamoto.

Akizungumza na Meneja wa Mkoa wa Morogoro Bw. Lwitiko Ndigha alipozuru Mkoa huo kukagua utendaji kazi, Hamad amewapongeza watendaji wa NHC kwa kazi nzuri wanazofanya na akawaelekeza kuzingatia maadili ya msingi ya Shirika ili kufikia malengo waliyowekewa. 

Mkurugenzi Mkuu  Hamad alipata fursa ya  kupitia mafaili kujiridhisha na maelekezo yanayotolewa kwa wabia ya kuzingatia taratibu za ujenzi. 

Ameandamana na Wakurugenzi kadhaa wa NHC katika ziara hiyo  
Previous Post Next Post