BRELA YATOA WITO KWA WADAU WANAOPATA SHIDA YA MFUMO WA USAJILI LESENI KUTEMBELEA BANDA LAO KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Wakala wa usajili wa biashara na leseni RELA Bi. Roida Andusamile akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendeleakwenye viwanja vya Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Sabasaba.

Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Wakala wa usajili wa biashara na leseni RELA Bi. Roida Andusamile akimkabidhi cheti cha usajili Afisa Mawasiliano wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi. Agustina Makoye mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili 

Na Humphrey Msechu

Wakala wa usajili wa biashara na leseni Brela imetoa wito Kwa wadau mbalimbali wanaopata shida katika mfumo wa uombaji leseni wanapaswa kufika kwenye Banda lao lilipo kwenye maonyesho ya 47 ya biashara Saba Saba ili kasaidiwa kutatua changamoto hizo.

Akizungumza Leo July 3 kwenye maonyesho hayo mkuu wa kitengo Cha mawasiliano Roida Andusamile amesema kuwa wamejipanga kuhudumia wananchi na kutoa elimu mbalimbali ikiwemo umiliki ubunifu.

Amesema nchi imekuwa na wabunifu wengi ambao awafaidiki na bunifu zao Kwa sababu ya kutokusajili bunifu hizo.

Kuna watu wanabuni vitu vingi lakini hawajua kama Kuna Brela wangeweza kuja kusajili vumbuzi zao na kuzilinda kisheria na kuweza kunufaika na hizo vumbuzi zao” amesema Andususamile

Aidha Andusamile ameongeza kuwa Taifa limekuwa na vijana wengi wasomi ambao wangeweza kujiajili na kuajili wengine Kwa kutumia vumbuzi zao.

Sambamba na hayo amesema kuwa uwepo wa brela kwenye maonyesho hayo ni kutoa elimu Kwa wananchi jinsi ya kumiliki leseni za biashara ndogo kubwa na za Kati ikiwemo viwanda.

“Kwenye maonyesho haya tunatoa elimu Kwa umma jinsi ya kumiliki leseni zao za biashara na kujisajili kupitia njia ya mtandao lakini pia kuwaelewesha wananchi kuhusu BRELA na shughuli tunazofanya hivyo wananchi watutembelee wapate elimu”ameongeza Andusamile
Previous Post Next Post